Waziri Ummy Mwalimu Awapongeza Viongozi Halmashauri Ya Temeke
HomeHabari

Waziri Ummy Mwalimu Awapongeza Viongozi Halmashauri Ya Temeke

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewapongeza viongozi wa Tem...

Tanzania Yakusudia Kutengeneza Chanjo Zake Zenyewe
Morocco Yakubali Kushiriana Na Tanzania Kwenye Michezo
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo February 16


Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewapongeza viongozi wa Temeke, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mkurugenzi pamoja na watumishi kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kusimamia miradi ya maendeleo.

Ametoa kauli hiyo leo Novemba 15,2021 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na benki ya Dunia, kupitia miradi ya kimkakati ya uendelezaji wa jiji la Dar es Salaam (DMDP).

Miradi hiyo ambayo ilikua kwenye awamu ya kwanza ya utekelezwaji wake, kwa sasa imekamilika na imekua chachu kubwa ya maendeleo na faida kwa Wananchi,huku zaidi ya bilioni 650 zikiwa zimetumika katika utekelezwaji wake kwa manispaa ya Temeke.

Waziri Ummy alitabanaisha kwamba kupitia fedha za benki ya Dunia, katika kuboresha huduma za jamii ,miundombinu ya Dar es Salaam ikiwemo kujenga barabara,vituo vya afya na masoko,maeneo mengi katika jiji yamebadilika na kupendeza.

Aidha amewashukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano huo,mbali na shukrani hizo, amewaomba kwamba katika awamu zijazo,waongeza ushirikiano katika kuboresha maeneo mengine ambayo bado hayajafikiwa na mradi huo.

Katika ziara hiyo Ummy amewangozana na viongozi mbalimbali wa benki ya Dunia akiwemo Mari Pangestu ambaye ni mkurugenzi wa sera, maendeleo na ushirikiano wa benki hiyo. Kwa pamoja walitembelea soko la Makangarawe na kituo cha afya Buza.

“Sekta ya afya imeimarika, vituo vipo vizuri, visafi, lakini tangu kituo hicho kimeanza kutoa huduma, hawajapata kifo kinachotokana na ujauzito au uzazi, kwa hilo amewapongeza sana,”amesema Waziri Ummy.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Ummy Mwalimu Awapongeza Viongozi Halmashauri Ya Temeke
Waziri Ummy Mwalimu Awapongeza Viongozi Halmashauri Ya Temeke
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgeAdoeWOn0FVrHAAOZK0a7nk4zVHElcZQ5dGl23B4SaZscAZowQXvp-E2afuL3cFVDHAkoHuCTYJsLdRqiEsWXVUgUxoehSNcygkR4ua_L6nMKl4Knvp-DN8nRq6HgtvCAeTk9nosqIH-SC-HAFPrnN2x3x-1fmcLqL_Wk47vPPUMhyKD9FOyTr5BLCw=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgeAdoeWOn0FVrHAAOZK0a7nk4zVHElcZQ5dGl23B4SaZscAZowQXvp-E2afuL3cFVDHAkoHuCTYJsLdRqiEsWXVUgUxoehSNcygkR4ua_L6nMKl4Knvp-DN8nRq6HgtvCAeTk9nosqIH-SC-HAFPrnN2x3x-1fmcLqL_Wk47vPPUMhyKD9FOyTr5BLCw=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/waziri-ummy-mwalimu-awapongeza-viongozi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/waziri-ummy-mwalimu-awapongeza-viongozi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy