Dkt.Samia apongeza wadau wanaopeleka gesi maeneo yote ya vijijini
HomeHabariTop Stories

Dkt.Samia apongeza wadau wanaopeleka gesi maeneo yote ya vijijini

RAIS DK.Samia Suluhu Hassan ameipongeza Kampuni ya Oryx Gas pamoja na wadau wengine kwa kuendelea kushiriki kikamilifu katika kampeni ya nis...

RAIS DK.Samia Suluhu Hassan ameipongeza Kampuni ya Oryx Gas pamoja na wadau wengine kwa kuendelea kushiriki kikamilifu katika kampeni ya nishati safi ya huku akitoa rai ya wadau hao kupeleka gesi katika maeneo ya vijijini.

Ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la Oryx Gas wakati wa uzinduzi wa kampeni ya matumizi nishati safi ya kupikia Kitaifa iliyozinduliwa katika viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza mkoani Tanga.

“Mitungi ya gesi inapoisha inabaki ndani kama feniture (Samani za ndani) ,hivyo nimeomba sekta binafsi na nimekutana na Oryx Gas pamoja na wadau wengine wakanihakikishia wataendelea kuipeleka mitungi ili wananchi waendelee kutumia.”amesema Rais Samia huku akiipongeza Oryx Gas.

Awali akitoa maelezo kwa Rais Samia, Meneja Miradi ya Nishati Safi ya Kupikia kutoka Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya jitihada mbambali za kuunga mkono kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini na

mkakati wao ni kuona kila nyumba inakuwa na mtungi wa gesi ya kupikia.

“Tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa ajenda yake ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Oryx Gas tumekuwa wadau wakubwa na tumefanya jitihada nyingi tokeo ilipotangazwa kama ajenda rasmi ya nchi kwamba wananchi tuanze kutumia nishati safi ya kupikia

“Tumeongeza miundombinu ya kusambaza mitungi ya Oryx Gas hasa katika maeneo ya vijiji ambapo kwa sasa huwezi kuikosa Oryx gas. mitungi ya Oryx inapatikana kila miji,Wilaya na vijijini pia tupo .Pia tumekuwa tukishiriki katika shughuli za mbalimbali za kuwezesha ukuaji wa matumizi ya nishati safi ambapo tumeweza kuisaidia jamii mbalimbali ikiwemo ya Wanawake kwa kuiwezesha kufikia hayo malengo.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan (kushoto) akızungumza na maofisa wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania baada ya kufika katika banda la Oryx wakati wa uzinduzi wa kampeni ya matumizi ya nishati safi kitaifa uliofanyika katika Viwanja vya CCM Jitegemee wilayani Muheza mkoani Tanga.Rais yuko Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi

The post Dkt.Samia apongeza wadau wanaopeleka gesi maeneo yote ya vijijini first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/cWu1R4r
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt.Samia apongeza wadau wanaopeleka gesi maeneo yote ya vijijini
Dkt.Samia apongeza wadau wanaopeleka gesi maeneo yote ya vijijini
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/03/IMG-20250302-WA0010-950x559.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/03/dktsamia-apongeza-wadau-wanaopeleka.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/03/dktsamia-apongeza-wadau-wanaopeleka.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy