Rais Samia asikia kilio cha tozo ya miamala ya simu, Atoa maelekezo kwa Waziri wa Fedha
HomeHabari

Rais Samia asikia kilio cha tozo ya miamala ya simu, Atoa maelekezo kwa Waziri wa Fedha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha inayashughulia malalamiko...

Waziri Kijaji: Tanzania Itaendeleza Ushirikiano Wa Kibiashara Kati Ya Tanzania Na Uingereza
Tanzania Kuwavutia Wawekezaji Kwenye Siku Ya Tanzania Maonesho Ya Expo 2020 Dubai
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo February 2


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha inayashughulia malalamiko yote yanayotolewa na Watanzania kuhusu tozo mpya za miamala ya simu zilizoanza kutumika Jula 15 mwaka huu.


Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba, hii leo Julai 19, 2021, akitoa tammko la serikali akiwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Faustine Ndugulile na kuwaomba Watanzania kuwa watulivu kwani serikali inafanyia kazi malalamiko yote.

“Tayari Mheshimiwa Rais ameshaguswa na jambo hili amesikia maoni ya Watanzania wote na amesema tuyafanyie kazi jambo hili.

“Kwa hiyo,nitoe rai kwa wananchi kuwa Serikali imesikia malalamiko ya wananchi na tayari tumeendelea kuyafanyia kazi, Waziri Mkuu ameshaitisha kikao kesho kuendelea kupitia masuala haya haya.


“Nitoe rai kwa wananchi kuwa watulivu kwenye jambo hili, tutaendelea kufafanua kwenye maeneo ambayo yanahitaji ufafanuzi na tutachukua hatua kwenye maeneo ambayo yanahitaji kuchukuliwa hatua "Amesema Waziri Nchema.


Huku akitaka sheria ziheshimiwe, Waziri Mwigulu ameonya watu wanaopotosha jambo hilo na kuwataka wananchi kuwa watulivu.

“Nitoe rai kwa ambao wanapenda kupotosha au kubadili dhana ya jambo ambalo limekusudiwa na lina maslahi mapana ya Taifa letu wasifanye hivyo. Sheria za nchi zinapaswa ziheshimiwe, hakuna haja ya kuwasikiliza wapotoshaji."

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile amesema; “Niwasihi Watanzania tuwe watulivu wakati jambo hili linafanyiwa kazi, Serikali yetu ni sikivu, na itaenda kulifanyia kazi jambo hili kuhakikisha tunafikia mwafaka mzuri"



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia asikia kilio cha tozo ya miamala ya simu, Atoa maelekezo kwa Waziri wa Fedha
Rais Samia asikia kilio cha tozo ya miamala ya simu, Atoa maelekezo kwa Waziri wa Fedha
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0oUh4mw_oNsVdOiIVq50T6vsMdmuAsB4Sp-FuqxmrZMKr2HFa63ZGECIlP986ygzZJV63aUNv3shPRbgn8xuOH_fpZIMXwmZyc-1fiDT2CFYWx2DE4boqmLqLQ0Clto57hXi0CuGIh2FL/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0oUh4mw_oNsVdOiIVq50T6vsMdmuAsB4Sp-FuqxmrZMKr2HFa63ZGECIlP986ygzZJV63aUNv3shPRbgn8xuOH_fpZIMXwmZyc-1fiDT2CFYWx2DE4boqmLqLQ0Clto57hXi0CuGIh2FL/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/rais-samia-asikia-kilio-cha-tozo-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/rais-samia-asikia-kilio-cha-tozo-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy