BAADA YA MOHAMED NA BOCCO KUONGEZA MKATABA, SASA NI ZAMU YA KAPOMBE
HomeMichezo

BAADA YA MOHAMED NA BOCCO KUONGEZA MKATABA, SASA NI ZAMU YA KAPOMBE

 IMEELEZWA kuwa baada ya mabosi wa Simba kumalizana na manahodha wao kwa kuwaongezea mikataba mipya sasa ni zamu ya beki wa pembeni Shomar...

NABI ANATAKA MABAO MENGI MBELE YA RIVERS UNITED
DEMBELE KUPEWA DILI JIPYA BARCELONA
FAMILIA YA MICHEZO YAMLILIA HANSPOPE, PUMZIKA KWA AMANI

 IMEELEZWA kuwa baada ya mabosi wa Simba kumalizana na manahodha wao kwa kuwaongezea mikataba mipya sasa ni zamu ya beki wa pembeni Shomari Kapombe.

Nahodha Mkuu, John Bocco mwenye mabao 10 ndani ya ligi msimu huu pamoja na nahodha msaidizi Mohamed Hussein mwenye mabao mawili ndani ya ligi jana walitambulishwa rasmi na Simba kwamba wameongeza mikataba yao.

Baada ya nyota hao kuongeza inaelezwa kwamba tayari wamekamilisha mazungumzo na Kapombe ambaye naye mkataba wake unafika ukingoni.

"Simba wanajambo lao kwa sasa hawapo tayari kuwaacha wachezaji ambao wapo kwenye mpango wao. Unaona kwamba tayari Mohamed na Bocco wameshatambulishwa na kuoneshwa kwa mashabiki basi kuna wengine wanafuata ikiwa ni pamoja na Kapombe.


"Kapombe naye mkataba wake unaisha msimu utakapokamilika hivyo mazungumzo yanakwenda vizuri na muda wowote naye atasaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia timu hiyo.

"Orodha ni ndefu kwani wachezaji wengi mikataba yao kwa sasa inafika ukingoni, hata Mkude, (Jonas) naye kandarasi yake ipo ukingoni, Mzamiru, (Yassin) ni suala la kusubiri," ilieleza taarifa hiyo.

Mohamed alikuwa anatajwa kuingia rada za timu za Afrika Kusini pamoja na Bongo ambapo watani zao wa jadi Yanga walikuwa wanatajwa kuwania saini yake.

Hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes aliweka wazi kwamba hatakubali kuona mchezaji anayemhitaji akiondoka ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kikiwa kimetinga hatua ya robo fainali.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: BAADA YA MOHAMED NA BOCCO KUONGEZA MKATABA, SASA NI ZAMU YA KAPOMBE
BAADA YA MOHAMED NA BOCCO KUONGEZA MKATABA, SASA NI ZAMU YA KAPOMBE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjK41yXUaPUiSlPpeXFxmjEg2XLu2gPYqm9wFRS7ZXghMPaf8YSqhlA6LY3mDxONsZo_BQN3uyXK4760D3fmil4xBmn6Up0I7GxnjaCV6U16tELciFNGSgcjJM5DdkzaBz_vmc1sAi0Ss9G/w640-h410/Kapombe+Goal.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjK41yXUaPUiSlPpeXFxmjEg2XLu2gPYqm9wFRS7ZXghMPaf8YSqhlA6LY3mDxONsZo_BQN3uyXK4760D3fmil4xBmn6Up0I7GxnjaCV6U16tELciFNGSgcjJM5DdkzaBz_vmc1sAi0Ss9G/s72-w640-c-h410/Kapombe+Goal.JPG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/baada-ya-mohamed-na-bocco-kuongeza.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/baada-ya-mohamed-na-bocco-kuongeza.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy