Rais Samia Aruhusu Kupandishwa Vyeo Maafisa, Wakaguzi Na Askari 34,106 Wa Vyombo Vya Ulinzi Na Usalama
HomeHabari

Rais Samia Aruhusu Kupandishwa Vyeo Maafisa, Wakaguzi Na Askari 34,106 Wa Vyombo Vya Ulinzi Na Usalama

Na Mwandishi Wetu MOHA. WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameruhusu kupandishwa vy...

Mganga Mkuu Wa Serikali Ahimiza Watumishi Wa Afya Kufanya Kazi Kwa Bidii
Rais Samia Arejea Dodoma Kutoka Ziara Ya Kikazi Ya Siku Mbili Nchini Msumbiji
Tanzania Na Poland Zaingia Makubaliano Ya Kuimarisha Huduma Ya Majisafi Na Usafi Mazingira


Na Mwandishi Wetu MOHA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameruhusu kupandishwa vyeo Maafisa, Wakaguzi na Askari 34,106, wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara yake kwa mujibu wa taratibu na sheria.

Akizungumza na Waandshi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dodoma, jana, Simbachawene alisema idadi hiyo ya waliopandishwa vyeo ni kubwa na haijawahi kutokea katika historia ya Wizara hiyo ambayo inaongoza vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji.

“Katika kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tayari Wizara yetu imewapandisha vyeo Maafisa, Wakaguzi na Askari wa ngazi mbalimbali 34,106 waliostahili kupandishwa vyeo katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2018/2019, 2019/2020 na 2020/2021,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi limewapandisha vyeo jumla ya Maafisa, Wakaguzi na Askari 26,464, Jeshi la Magereza, limewapandisha vyeo jumla ya Maafisa, Wakaguzi na Askari 6,310, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 149, na Idara ya Uhamiaji, imewapandisha vyeo 1,183 ambapo kwa jumla ya vyombo vyote inafikisha idadi ya waliopandishwa vyeo kuwa 34, 106.

Aidha, Waziri Simbachawene amesema Rais Samia ametoa fedha kwa ajili kwenda kwenye mafunzo mbalimbali na kuanzia sasa matangazo yatakua yakitolewa kwa kada tofauti kwenda kwenye vyeo, na mafunzo hayo yatafanyika kwa miezi sita na miezi mitatu.

Waziri Simbachawene aliwapongeza Maafisa, Wakaguzi na Askari wote waliopandishwa vyeo na aliwataka kufanya kazi kwa bidii, weledi na nidhamu kwa kufuata sheria za kazi na kuepuka vitendo vya rushwa kwa maendeleo ya Taifa.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia Aruhusu Kupandishwa Vyeo Maafisa, Wakaguzi Na Askari 34,106 Wa Vyombo Vya Ulinzi Na Usalama
Rais Samia Aruhusu Kupandishwa Vyeo Maafisa, Wakaguzi Na Askari 34,106 Wa Vyombo Vya Ulinzi Na Usalama
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg16mN4O_U7M3OpsfVHO1w_0VQSuZVSL8zUlW3QY9sr2rSh8PnCwdaWt4sPduq88uL6vVynV1Oqifdny-DjA5A4Z86i9h22oCSI6FBnUDOgH11-1IpMaqG25U12UZMqdB3y4EouGxmL6wdj/s16000/WhatsApp-Image-2021-06-11-at-2.13.11-PM.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg16mN4O_U7M3OpsfVHO1w_0VQSuZVSL8zUlW3QY9sr2rSh8PnCwdaWt4sPduq88uL6vVynV1Oqifdny-DjA5A4Z86i9h22oCSI6FBnUDOgH11-1IpMaqG25U12UZMqdB3y4EouGxmL6wdj/s72-c/WhatsApp-Image-2021-06-11-at-2.13.11-PM.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/rais-samia-aruhusu-kupandishwa-vyeo.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/rais-samia-aruhusu-kupandishwa-vyeo.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy