UCHAGUZI UMEKWISHA, SASA NI MUDA WA KAZI KUENDELEA
HomeMichezo

UCHAGUZI UMEKWISHA, SASA NI MUDA WA KAZI KUENDELEA

BAADA ya tukio la uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), ambalo lilihusisha nafasi ya Urais pamoja na nafasi za Wajumbe wa ...

NEYMAR JR AFIKIRIA KUSTAAFU
SIMULIZI YA BINTI ALIYEKUWA NA MAWAZO KUHUSU ISHU YA MAPENZI
VIDEO:NYOTA TWIGA STARS AKIRI KUWA MASHINDANO YALIKUWA MAGUMU


BAADA ya tukio la uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), ambalo lilihusisha nafasi ya Urais pamoja na nafasi za Wajumbe wa Kamati Tendaji ambao walikuwa wanapambana kupata nafasi ya kuziwakilisha kanda zao sasa acha kazi iendelee.


Kabla ya uchaguzi wenyewe kufanyika ni wazi ilikuwa imeshajulikana kuwa Wallace Karia alikuwa anasubiri kuthibitishwa tu kama Rais wa  TFF kutokana na kuwa mgombea pekee aliyekidhi vigezo vyote kwenye nafasi ya Urais.

Kulikuwa na vigingi vingi kuelekea uchaguzi huu, wapo ambao walidiriki kutinga mahakamani kuzuia mchakato mzima wa uchaguzi kwa kile walichoeleza kuwa ulikiuka baadhi ya kanuni lakini jambo la kheri ni kuwa yote yaliisha na ratiba ya uchaguzi ikabaki palepale na tayari Wallace Karia alifanikiwa kutetea kiti chake kwa muhula wa pili ambapo atadumu madarakani kwa miaka minne akiliongoza Shirikisho hilo.


Kwa sasa uchaguzi umeisha hivyo ni wazi tunapaswa kujikita katika kupambania maendeleo ya mpira wetu ambao kwa kiasi kikubwa unaendelea kukua kadri siku zinavyozidi kusogea. Masuala ya migogoro ambayo haina afya na mustakabali wa maendeleo ya mpira wetu kwa sasa hayana nafasi kinachopaswa kufanyika ni kumuunga mkono Rais Karia ili mpira wetu uzidi kusonga mbele.


Rais Karia ni miongoni mwa viongozi pekee waliofanya makubwa kwenye miaka minne ya kwanza akiwa Rais wa shirikisho, kuanzia ngazi ya klabu hadi kwenye timu za taifa, chini ya utawala wake tumeshuhudia mafanikio makubwa kwenye timu za taifa za wakubwa, vijana na timu za wanawake.

Chini ya uongozi wake ameinyanyua na kuipa thamani Ligi ya Wanawake haya ni miongoni mwa machache ambayo Rais Karia alianza nayo na kwa kiasi kikubwa amefanikiwa. Hivyo basi tuungane kwa pamoja kuendeleza safari hii ambayo aliianzisha kwenye muhula wa kwanza kwenye uongozi wake.


Wajumbe wa kamati tendaji kutoka kanda mbalimbali ambao pia mmepata nafasi ya kushinda kwenye kinyang’anyiro ni muda wenu kuwa wasaidizi bora kwa Rais Karia kwenye kanda mnazotoka mnapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha soka linakuwa kutoka kila kona ya nchi.

Kwa wale ambao walikwazika kwenye kipindi cha mchakato wa uchaguzi, ni muda wa kuungana pamoja kwani lengo lenu lilikuwa ni moja nalo ni kuhakikisha mpira wetu unasonga mbele, haina haja ya kuendeleza malumbano ambayo hayatakuwa na tija yoyote kwenye mpira wetu, kama hukufanikiwa kuubadilisha mpira ukiwa ndani ya shirikisho unaweza kuubadilisha hata ukiwa nje ya shirikisho kupitia maoni na ushauri wenye tija.


Leo tunashuhudia Ligi Kuu Bara ikishika nafasi ya nane kwa ubora barani Afrika, hili ni la kujivunia kwani siyo rahisi kwa ligi yetu kufikia hapo kama kusingekuwa na utawala bora kwenye shirikisho letu. Kila la heri Rais Karia.

Jikiteni kwenye ushindani wa kibiashara kunufaisha timu zenu.


 



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: UCHAGUZI UMEKWISHA, SASA NI MUDA WA KAZI KUENDELEA
UCHAGUZI UMEKWISHA, SASA NI MUDA WA KAZI KUENDELEA
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEibefVcvxEGKhgtcXxZPYwEcntwiii0iAbkhiZ5-IDycaK-CW2jWVECeAjgGmlMj94VwLF4kAiGC3NghPzeVVCDe8gax0svFAuoipT3ad75oj-10tv-JiABtneYE6umI7AcsQOc0XDw5o7LLYmOr8lRNZwSvud800H2OszWVeZuxUBwh_Vd8feGvtJYEA=w640-h426
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEibefVcvxEGKhgtcXxZPYwEcntwiii0iAbkhiZ5-IDycaK-CW2jWVECeAjgGmlMj94VwLF4kAiGC3NghPzeVVCDe8gax0svFAuoipT3ad75oj-10tv-JiABtneYE6umI7AcsQOc0XDw5o7LLYmOr8lRNZwSvud800H2OszWVeZuxUBwh_Vd8feGvtJYEA=s72-w640-c-h426
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/uchaguzi-umekwisha-sasa-ni-muda-wa-kazi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/uchaguzi-umekwisha-sasa-ni-muda-wa-kazi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy