Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akiwasilisha mada katika semina kwa watendaji wa Serikali kuhusiana na changamoto ...
Baadhi ya watendaji wa Serikali kutoka idara za mahakama, maofisa wa Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi pamoja na wanasheria walioshiriki katika semina hiyo iliyofanyika Double View Hoteli jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya watendaji wa Serikali kutoka idara za mahakama, maofisa wa Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi pamoja na wanasheria walioshiriki katika semina hiyo iliyofanyika Double View Hoteli jijini Dar es Salaam. |
Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi akiwasilisha mada katika semina
kwa watendaji wa Serikali kuhusiana na changamoto za kesi za ukatili wa
kijinsia.
Baadhi ya watendaji wa Serikali kutoka idara za mahakama, maofisa wa Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi pamoja na wanasheria walioshiriki katika semina hiyo iliyofanyika Double View Hoteli jijini Dar es Salaam. |
MTANDAO
wa Jinsia Tanzani TGNP umekutanisha baadhi ya watendaji wa Serikali
kutoka idara za mahakama, maofisa wa Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi
la Polisi pamoja na wanasheria kujadili changamoto ya masuala ya sheria
na sera katika kesi za ukatili wa kijinsia.
Semina
hiyo kwa watendaji wa Serikali pia ilijadili nafasi za watendaji wa
Serikali katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ngazi ya
jamii na kutoa mapendekezo ya baadae kukabiliana na changamoto hizo
Akizungumza
katika semina hiyo akiwasilisha mada, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP
Mtandao, Lilian Liundi alisema mfumo dume umeathiri jamii hivyo matendo
mengi yanayofanywa kwa wanawake na wanaume kutegemeana na mtazamo wa
jinsi zao na kuwa katika upendeleo zaidi na siyo katika nafasi ya usawa
katika jamii.
“…Huu ni mfumo wala si mwanamke au mwanamme, ila ni mfumo unaohodhi madaraka, maamuzi, rasilimali nk.
Wengi
huhusisha na ubabe, uonevu na ukatili ambapo katika mazingira halisi
ubabe unafanywa sana na wanaumme,” alisema Bi. Liundi.
Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC) cha TAMWA, Glagness Munuo akiwasilisha mada katika semina hiyo
Aidha
alisema lipo pengo la kijinsia tofauti; kitabia, ubora au kwa kiasi ya
kutendewa kati ya wanaume na wanawake, na mara nyingine wasichana na
wavulana kuhusiana na fursa za rasilimali/mali/huduma mahitaji, nafasi
na mahitaji ya msingi katia jamii.
“…Majukumu
ya kijinsia ni mitizamo inayojengeka katika familia/jamii kuhusu
shughuli/majukumu ya wanawake na wanaume ambapo shughuli/majukumu fulani
yanaoneka ni ya wanawake na mengine ni ya wanaume. Mitazamo hii
inajengeka na kuathiriwa na umri, mila na tamaduni, dini, mazingira na
mabadiliko ya kiuchumi, na kisiasa; kukua kwa maendeleo, sera za kijamii
na kiuchumi…,” alisema
Aliongeza
kuwa licha ya wanawake na wanaume wote wanashiriki katika shughuli za
uzalishaji lakini kazi na shughuli azifanyazo mwanamke hazionyeshi
matokeo yake waziwazi kama zile azifanyazo mwanaume katika jamii hali
inayosababisha kupuuzwa kwa mchango wake katika jamii.
“…Mwanaume
anakuwa na kazi ambazo nyingi ni rasmi kama vile uongozi na majukumu
yake, na vile vile kufanya kazi zenye hadhi ya juu ukilinganisha na
mwanamke anayefanya kazi nyingi za kuhudumia
Majukumu
haya ni zile kazi ambazo wanajamii wanazifanya ili kuhakikisha
upatikanaji na kuwepokwa vitu muhimu katika kuendeleza jamii, kwa mfano
huduma za pamoja kama vile maji, huduma ya afya, elimu,” aliongeza
Mkurugenzi huyo.
Baadhi ya watendaji wa Serikali kutoka idara za mahakama, maofisa wa Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi pamoja na wanasheria walioshiriki katika semina hiyo iliyofanyika Double View Hoteli jijini Dar es Salaam. |
Kwa
upande wake Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi (CRC) cha TAMWA, Glagness
Munuo akiwasilisha mada katika semina hiyo alisema ukatili wa kijinsia
ni jambo ambalo linawanyima uhuru wanaume, wanawake na watoto kufurahia
haki za msingi za kibinadamu na kufanya wapendayo.
Aliongeza
kuwa ukatili wa kijinsia unatokana na tofauti za kijinsia na baadhi ya
mila na desturi potofu ambazo husababisha kuwepo kwa tofauti za kijinsia
katika ngazi mbalimbali za jamii. Aidha alibainisha kuwa ukatili wa
kijinsia unaendelea kufichwa kwa sababu unaonekana kuwa ni kitendo cha
siri ambacho mtu mwingine hastahili kukifahamu.
Hata
hivyo kutokana na kuwepo wanaharakati na vyombo vya habari suala la
ukatili wa kijinsia kuliweka bayana inaeleweka zaidi kwa watu. Aliyataja
madhara ya vitendo vya ukatili kuwa ni pamoja na wahusika kujeruhiwa
vibaya, ulemavu, kifo, magonjwa ya zinaa na Ukimwi Matatizo ya afya ya
uzazi. Mengine ni pamoja na Mimba kuharibika kwa akinamama, Hofu,
Kutokwa na damu nyingi, Mimba zisizotarajiwa.
COMMENTS