HII NDIYO A - Z YA BINTI MCHAWI ALIYEDONDOKA KWA CHUNGU KUTOKA ANGANI MJINI SHINYANGA
HomeMatukio

HII NDIYO A - Z YA BINTI MCHAWI ALIYEDONDOKA KWA CHUNGU KUTOKA ANGANI MJINI SHINYANGA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida binti anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23- 25 anayedaiwa kuwa ni mchawi amekutwa kwenye nyumba ya m...

Wema Hajampeleka Diamond Mahakamani – Martin Kadinda Akanusha
WALIMU MBEYA WAANDAMANA KUDAI HAKI ZAO
Lulu amtaka Marlaw kurudi kwenye game




Katika hali isiyokuwa ya kawaida binti anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 23- 25 anayedaiwa kuwa ni mchawi amekutwa kwenye nyumba ya mtu katika mtaa wa Bushushu kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga akiwa amevaa kishirikina na mwili wake ukiwa umepakwa dawa nyeusi akidai alikuwa anaongoza wenzake zaidi ya 10 kutoka kanda ya ziwa kuwanga katika nyumba hiyo.



Tukio hilo lililovuta hisia za mamia ya wakazi wa Shinyanga limetokea jana asubuhi nyumbani kwa Robinson Massawe ambapo binti huyo alikutwa amelala mbele ya mlango wa nyumba hiyo akiwa hajitambui na baada ya kusemeshwa ndipo akasimulia yaliyomkuta kwamba alifika mahali hapo na wenzake zaidi ya 10 kufanya sherehe baada ya kufanikisha uchawi wao.



Mashuhuda wa tukio walisema baada ya kumhoji binti huyo alisema alifika kwenye familia hiyo,akiwa kiongozi wa kundi la wachawi zaidi ya 10 kutoka Ushirombo,Misungwi na Shinyanga saa 9 usiku kwa ajili ya kufanya sherehe baada ya kufanikiwa kusambaratisha kichawi ndoa ya Massawe na Mary Joseph.



“Tumemkuta hapa anasema leo ni mara ya tatu wanakuja kufanya uchawi wao,lengo lao ni kutaka ndugu yao aolewe na Massawe,walikuja siku ya kwanza wakakuta mke wa Massawe akisali,wakashindwa,wakarudi mara ya pili kwa ajili ya kusambaratisha ndoa,wakafanikiwa leo walikuja kufanya sherehe kwa kazi hiyo lakini wenzake wamemkimbia”,alieleza Stella Joseph mdogo wa mke aliyeachika.



“Anadai kuwa Robinson alitoa ahadi ya kumuoa mwanamke ambaye ni ndugu yao badala yake akaoa mwanamke mwingine,aliyeahidiwa kuolewa katoa taarifa kwa mama mdogo wake ambaye ni mchawi,naye kalifikisha kwa wakuu wake,wakaamua kuingia kazini kutaka ndoa kishirikina”,aliongeza Hamis Juma.



Akizungumza na Malunde1 blog iliyofika eneo la tukio haraka sana tena kawaida yake,binti huyo anayedaiwa kuwa mchawi aliyejitambulisha kwa jina la Coletha akizugumza kwa lugha ya Kisukuma kutoka Ushirombo mkoani Geita, alisema alikuwa anaongoza kundi la wachawi kutoka Mwanza,Geita na Shinyanga lakini wakazidiwa nguvu wenzake wakamkimbia.



“Mimi ni mdogo sana kwa wachawi wenzangu,siyo mzoefu sana,walinitanguliza mbele ,nilipodondoka na chungu change wenzangu wakanikimbia,nimebaki peke yangu,kila mmoja amekuja na usafiri wake,mimi nimekuja na chungu,wengine wamekuja na ungo”,alieleza Binti huyo.

"Baba mwenye nyumba hii alitoa ahadi ya kuoa mtoto wa mshirika mwenzetu(mama mdogo wa binti),na mama mdogo huyo ndiyo akaleta malalamiko kwa wachawi kuwa tumshughulikie huyu baba anayechezea watoto wa watu",aliongeza.



Naye mwenyekiti wa mtaa wa Bushushu Ruben Masanja aliyefika eneo la tukio alisema ni kweli ndoa ya Robinson na Mary imevunjika tangu mwezi Septemba mwaka 2014 na sasa baba wa familia hiyo anaishi na ndugu zake.



Masanja aliongeza kuwa huenda binti huyo ni mchawi kutokana na maelezo yake na vitendo vilivyotokea katika familia hiyo huku akiwasihi wakazi wa eneo hilo kutomwadhibu binti huyo kisha kumwingiza ndani ya nyumba kusubiri polisi kwa ajili ya usalama wake.



“Anasema walikuja kufanya sherehe baada ya kumaliza kazi ya kuvuruga ndoa,na kweli wanandoa wametengana tangu tarehe 17 Septemba 2014,sasa wachawi hao wanataka ndugu yao aliyeahidiwa kuolewa na Robinson aolewe,binti anayetaka kuolewa alitoa taarifa kwa mama mdogo wake ambaye ni mchawi,huyo mama akatoa taarifa kwa wachawi wenzake ili washughulikie suala hilo”,Masanja aliiambia Malunde1 blog



Hata hivyo katika hali ya kushangaza watu mwanzo kufika katika eneo la tukio walitoweka na vipande vya chungu alichodondoka nacho binti huyo.



Kufuatia tukio hilo askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga walifika eneo la tukio na kumchukua binti huyo kwenye gari la polisi.



Tukio hili la binti kukutwa akiwanga nyumbani kwa mtu limetokea siku chache tu baada ya bibi asiyejulikana makazi yake mwenye umri wa miaka 80 kukutwa uchi nje ya nyumba ya mtu katika kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde-Shinyanga




Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: HII NDIYO A - Z YA BINTI MCHAWI ALIYEDONDOKA KWA CHUNGU KUTOKA ANGANI MJINI SHINYANGA
HII NDIYO A - Z YA BINTI MCHAWI ALIYEDONDOKA KWA CHUNGU KUTOKA ANGANI MJINI SHINYANGA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiHtANI8BEEM0S9O0mRnZ_RXmohxIzA4ZFlgaPK5HayDoRMSfArTmFJo6ulB8tY_8w4MoAQwX1AhMOyRdUyOAlanxXZELMIOyDUTSH4Cu5JsS9ZHJBkGy80e920zFKTuLZJ5qlulgfqSrM/s640/3+(61).jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiHtANI8BEEM0S9O0mRnZ_RXmohxIzA4ZFlgaPK5HayDoRMSfArTmFJo6ulB8tY_8w4MoAQwX1AhMOyRdUyOAlanxXZELMIOyDUTSH4Cu5JsS9ZHJBkGy80e920zFKTuLZJ5qlulgfqSrM/s72-c/3+(61).jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/02/hii-ndiyo-z-ya-binti-mchawi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/02/hii-ndiyo-z-ya-binti-mchawi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy