Waziri Mulamula: Wafanyabiashara Changamkieni Fursa Za Masoko Katika Jumuiya Za Kikanda
HomeHabari

Waziri Mulamula: Wafanyabiashara Changamkieni Fursa Za Masoko Katika Jumuiya Za Kikanda

 WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ametoa rai kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kucha...

Maafisa Ugani Wote Lazima Wawe Na Mashamba Darasa-Majaliwa
Mradi Wa Umeme Wa Rusumo Kukamilika Mwezi Desemba, 2021
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aondolewa madarakani


 WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ametoa rai kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa za masoko zinazopatikana katika Jumuiya za Kikanda ambazo Tanzania ni mwanachama kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na fursa zitokanazao na Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA)

Waziri Mulamula ametoa rai hiyo wakati akizungumza na wafanyanyabisha kwenye maadhimisho ya kilele cha Maonesho ya Bukoba “Bukoba Expo" yaliyofanyika katika Viwanja ya CCM mjini Bukoba. Maonesho hayo yaliyobebwa na kauli mbiu isemayo “Biashara, viwanda na utalii ni fursa ya uwekezaji Mkoani Kagera”.

Akizungumza na wafanyabiashara wakati wa akifunga maonesho hayo Waziri Mulamula alieleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inayo dhamira ya dhati ya kukuza uchumi wa nchi kupitia biashara na uwekezaji kwa kudumisha ushirikiano na nchi jirani na kutafuta fursa za masoko kwa bidhaa zinazozalishwa nchini. Aliongeza kusema wakati Serikali inafanya hayo ni vyema sekta binafsi ikaunga mkono juhudi hizo za Serikali kwa kuchangamkia fursa za masoko zinazopatikana katika Jumuiya za Kikanda ili kujiongezea tija zaidi katika shughuli zao.

Mtakumbuka kuwa Tanzania pamoja na kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pia ni mwanachama wa SADC na hivi karibuni tumeridhia mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (Africa Continental Free Trade Area-AfCFTA). Eneo Huru la Biashara la Afrika ni soko kubwa kuliko masoko yote yaliyoanzishwa ulimwenguni kwa kuwa na uwingi wa nchi wanachama zinazofikia 55. Soko hili linakadiriwa kuwa na idadi ya watu wapatao Bilioni 1.3 na Pato ghafi la Taifa (GDP) lenye jumla ya Dola za Marekani trilioni 3.4 na fursa za uchumi unaokua kwa kasi. Alieza Waziri Mulamula

Akizungumzia kuhusu maonesho hayo Waziri Mulamula ameleeza kuwa ubunifu wa waandaji umeakisi maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Mkoa wa Kagera na wananchi wake wanapata maendeleo kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi, biashara na uwekezaji kwa kutumia fursa zilizopo katika Mkoa huo na nafasi ya Kijiografia ya Mkoa kwa kupakana na nchi za Rwanda, Burundi na Uganda.

Kwa upande wake mratibu na mwandaaji wa Maonesho ya Bukoba Bw. William Rutta ameeleza kuwa maonesho hayo ambayo yamewavutia washiriki zaidi ya 350 wakiwemo wajasiliamari, wafanyabiashara, Taasisi za serikali na washiriki kutoka nchi za Burundi, Uganda, na Congo yametembelewa na wateja zaidi ya 10,000.

Aidha Bw. Rutta amebainisha malengo ya amonesho hayo kuwa ni pamoja na kuweka mwendelezo wa wiki ya uwekezaji ya Kagera ya mwaka 2019, kuunganisha wafanyabiashara na wananchi wote kushiriki katika shughuli za kuzalisha, mali, kuendeleza utalii na kubadilishana teknolojia ya uzalishaji na kuhamasisha utalii kwa kuandaa safari katika mbuga za wanyama asili za Burigi, Ibanda kyerwa, Runanyika Karagawe, Hifadhi ya Rubondo, Seregeti na vivutio vya asili kama fukwe za ziwa Victoria. Lengo lingine ni uboreshaji wa mazingira kwa kuhamasishwa upandaji miti aina ya palm tree katika mji wa Bukoba.

Waziri Mulamula kwenye maadhimisho ya kilele cha maonesho hayo pamoja na wajumbe wengine aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja Jenerali, Charles Mbuge, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Moses Machali na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Bi. Costansia Guhiye.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Mulamula: Wafanyabiashara Changamkieni Fursa Za Masoko Katika Jumuiya Za Kikanda
Waziri Mulamula: Wafanyabiashara Changamkieni Fursa Za Masoko Katika Jumuiya Za Kikanda
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3a_0izFo1amkfYajzH3rFQ4MGunwZuxtNhhbhkS1lXl1-sK5lBvemKuRc_CFC6runk8JtZnskkbrnY6VBLUiK8qaJZ8Mym0plcs4BjOODjFir2yVy1199FNp6gHO77XNqXovX5W4ujTR7GB0EGFD6VweaLnbww5yazbKxzNLCVZTy-LzO6cGVEVfOwA/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3a_0izFo1amkfYajzH3rFQ4MGunwZuxtNhhbhkS1lXl1-sK5lBvemKuRc_CFC6runk8JtZnskkbrnY6VBLUiK8qaJZ8Mym0plcs4BjOODjFir2yVy1199FNp6gHO77XNqXovX5W4ujTR7GB0EGFD6VweaLnbww5yazbKxzNLCVZTy-LzO6cGVEVfOwA/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/waziri-mulamula-wafanyabiashara.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/waziri-mulamula-wafanyabiashara.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy