Mradi Wa Umeme Wa Rusumo Kukamilika Mwezi Desemba, 2021
HomeHabari

Mradi Wa Umeme Wa Rusumo Kukamilika Mwezi Desemba, 2021

Na Dorina G. Makaya - Ngara Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani amesema, Mradi wa Umeme wa Rusumo utakamilika Desemba, 2021. Wa...

Infinix Kuja na Toleo Jipya lenye ukubwa mara mbili zaidi ya matoleo ya awali.....Bofya Hapa Kujua Zaidi
Chuo Cha Ardhi Morogoro Chatakiwa Kuweka Mikakati Kukamilisha Urasimishaji Makazi
Waziri Mchengerwa Awataka Watumishi Wa Umma Kuacha Kiburi Na Majivuno Wanapotoa Huduma Kwa Wananchi

Na Dorina G. Makaya - Ngara
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani amesema, Mradi wa Umeme wa Rusumo utakamilika Desemba, 2021.


Waziri Kalemani ametoa taarifa hiyo tarehe 12 Juni, 2021 katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao cha pamoja cha Mawaziri wa nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi zinazohusika na Mradi wa Umeme wa Rusumo kilichofanyika katika eneo la mradi la Rusumo.


Waziri Kalemani ameeleza kuwa, Mawaziri wa nchi zote tatu zinazohusika na Mradi wa Rusumo, Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Ibrahim Uwizeye, Waziri wa Miundombinu Mhe. Balozi Claver Gatete  pamoja na yeye mwenyewe Waziri wa Nishati wa Tanzania,  wameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Rusumo ambao ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 80.


Aidha, Dkt. Kalemani amebainisha kuwa, handaki la kupitishia maji yanayotoka kwenye bwawa kwenda kwenye mitambo ya kuzalisha umeme lenye urefu wa mita 703 tayari limekamilika kwa asilimia 80 tarehe 12 mwezi Juni, 2021. 


Waziri Kalemani ameeleza kuwa, njia za kusafirisha umeme zitagharimu dola milioni 113.2 na kuwa, baada ya kukamilika ujenzi zitaokolewa dola milioni 25 ambazo zitatumika katika kujengea njia nyingine ya umeme kwa nchi zote tatu ili kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika nchi hizo.


Amebainisha kuwa, jumla ya shilingi bilioni 10 za kitanzania zimetumika kwa ajili ya miradi ya kijamii katika wilaya ya ngara kwa upande wa Tanzania, ambapo miradi hiyo inahusisha ujenzi wa vituo vya afya viwili, ujenzi wa zahanati mbili, ujenzi wa shule za sekondari 3, ujenzi wa shule za msingi mbili, ujenzi wa chuo cha ufundi stadi na ujenzi wa miradi miwili ya maji pamoja na miradi ya kilimo na ufugaji wa nyuki inayowanufaisha wakazi wa wilaya ya Ngara


Dkt. Kalemani ametoa wito kwa watumiaji wa maji ya mto Rubuvu na mto Kagera, kutumia maji ya mito hiyo kwa uangalifu pamoja na kutunza vyanzo vya mito hiyo ili Mradi wa Umeme wa Rusumo usipungukiwe na maji huku akibainisha kuwa, upo uwezekano wa kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme wa Mradi wa Umeme wa Rusumo .


Ziara hiyo ililenga kutembelea mradi huo na kuona maendeleo yake pamoja na kutoa maelekezo kwa wakandarasi  kuhusiana na umuhimu wa kukamilishwa kwa ujenzi wa Mradi huo kama ilivyopangwa. 


Mawaziri kutoka Tanzania, Rwanda na Burundi walitembelea  eneo linapojengwa Bwawa, ( Dam site), Eneo la kuzalisha umeme ( Power House), na Eneo la kupokea umeme kabla haujasambazwa ( Switch yard) na kuridhishwa na kasi ya ujenzi.


Waziri Kalemani amesema, Mradi wa Umeme wa Rusumo ni  muhimu sana na kukamilika kwake kutaondoa changamoto nyingi za umeme na kuwa baada ya kikao cha pamoja cha Mawaziri wa nchi zote tatu, wamewataka wakandarasi hao ifikapo mwezi Desemba, 2021 wawe wamekabidhi Mradi na wananchi waanze kutumia umeme unaotokana na Mradi huo wa Umeme wa Rusumo.


Mradi wa umeme wa Maporomoko ya maji Rusumo ulianza mwezi Machi 2017 na utazalisha MW 80 ambapo nchi tatu husika za Tanzania, Rwanda na Burundi zitapata mgao sawa wa MW 27 zitakazoingizwa kwenye gridi ya Taifa kwa kila nchi.


Katika ziara hiyo Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani, aliambata na Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO pamoja na Uongozi wa Serikali wa Wilaya ya Ngara.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mradi Wa Umeme Wa Rusumo Kukamilika Mwezi Desemba, 2021
Mradi Wa Umeme Wa Rusumo Kukamilika Mwezi Desemba, 2021
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgfO-CPggVTXNGKkRN4TFgtmdA7TwelpA2mfRoWgXSP9h3EjH0lZxcds3z1_YF1cyu9GJbnDnKQKV4gUVdLKMmAUEqks6PDUg7Bgi2HQ8htOFxLCwLOeBs4uysh-LWQkDkI2f7R4kuV6_ny/s0/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgfO-CPggVTXNGKkRN4TFgtmdA7TwelpA2mfRoWgXSP9h3EjH0lZxcds3z1_YF1cyu9GJbnDnKQKV4gUVdLKMmAUEqks6PDUg7Bgi2HQ8htOFxLCwLOeBs4uysh-LWQkDkI2f7R4kuV6_ny/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/mradi-wa-umeme-wa-rusumo-kukamilika.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/mradi-wa-umeme-wa-rusumo-kukamilika.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy