Majaliwa Amwakilisha Rais Samia Katika Mkutano Wa Jukwaa La Nne La Vijana Duniani
HomeHabari

Majaliwa Amwakilisha Rais Samia Katika Mkutano Wa Jukwaa La Nne La Vijana Duniani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Jukwaa la Nne la Vijana Duniani lililoanza leo jijin...

Dkt.Mpango: Serikali Inaendelea Kushughulikia Changamoto Za Wazee Hasa Kwenye Sekta Ya Afya
Wakurugenzi Halmashauri Watakiwa Kuboresha Ofisi Za Maafisa Ardhi
Ajali Yaua 22 Morogoro, Rais Samia Aomboleza


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Jukwaa la Nne la Vijana Duniani lililoanza leo jijini Sharm-El-Sheikh, Misri. 

Akishiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao  mchana (Jumatatu, Januari 10, 2022) kutoka ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma, Waziri Mkuu ameyaomba mataifa makubwa duniani yashirikiane na nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ili kuhakikisha uchumi wa nchi hizo unarejea katika hali yake ya kawaida kutokana na madhara ya UVIKO-19.

“Tangu kuingia kwa wimbi la kwanza la UVIKO-19, tumeshuhudia athari kubwa za kiuchumi na hasa kwa vijana. Vijana wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa nchi yetu lakini uwepo wa UVIKO-19 umeathiri maendeleo ya sekta ya utalii ambapo vijana wengi wameajiriwa.”

Ameongeza kuwa UVIKO-19 umeathiri uwekezaji katika viwanda na kwenye sekta ya miundombinu ambako makampuni mengi yalitoa ajira kwa vijana lakini hayakuweza kufanya kazi na hivyo kuleta athari kubwa.

Akitoa mfano, Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Samia alipata fursa ya kuzungumza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Marekani mwaka jana ambako alieleza athari za ugonjwa wa UVIKO-19 na Tanzania ikaweza kupata mkopo nafuu uliotumika kujenga madarasa na vituo vya afya kama njia ya kurejesha uchumi.

“Tumehamasisha Umoja wa Afrika (AU) ulichukue suala hili kama ajenda ili uweze kujadili namna bora ya kurejesha uchumi wa Afrika; Tanzania ikiwa mwanachama wa AU nayo pia itaingia kwenye mjadala huu na tutapata njia bora ya kurejesha uchumi wetu hasa tunapolikabili wimbi la nne.”

Amesema Tanzania imeonesha inahitaji kuungwa mkono katika jitihada zinazochukuliwa kwenye ujenzi wa miundombinu ili Watanzania na hasa vijana waweze kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na uchumi wa jumla wa kitaifa.

Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo ni Rais wa Misri, Bw. Abdel Fattah Al-Sisi, Rais wa Colombia, Bw. Ivan Derque Marques, Rais wa Romania, Bw. Klaus Iohannis, Rais wa Zambia, Bw. Hakainde Hichilema, Rais wa Malta, Bw. Malta George Vella na Waziri wa Nchi wa Falme za Kiarabu anayeshughulikia Masuala ya Vijana, Bi. Shamma al Mazrui.

Mkutano huo wa siku nne ambao unashirikisha wajumbe zaidi ya 5,000 kutoka nchi mbalimbali duniani, unalenga kujadili madhara ya UVIKO-19 kwa vijana na namna gani nchi zimeweka mikakati ya kukabiliana nazo katika shughuli za kiuchumi, mabadiliko ya tabia nchi, hifadhi za jamii, haki za binadamu na uhifadhi wa mazingira.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Majaliwa Amwakilisha Rais Samia Katika Mkutano Wa Jukwaa La Nne La Vijana Duniani
Majaliwa Amwakilisha Rais Samia Katika Mkutano Wa Jukwaa La Nne La Vijana Duniani
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiZg7CejH6lFj_7m1ACUMI5xRD2YpFn8_xi5Pbcd1t5gNM564orFONOrnLZL9h_SfERajnFtH8fUY3S0rR3UBz3r9yEu8wxcOnSeBVJc2DZoI68-xM1PE2MnnVEXb7aaj1AxnMwtwGodxAEnE5JoXBmZdwYsjgLKLl6vU4pP4Vd0f4GSYyGOoCptNfwlg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEiZg7CejH6lFj_7m1ACUMI5xRD2YpFn8_xi5Pbcd1t5gNM564orFONOrnLZL9h_SfERajnFtH8fUY3S0rR3UBz3r9yEu8wxcOnSeBVJc2DZoI68-xM1PE2MnnVEXb7aaj1AxnMwtwGodxAEnE5JoXBmZdwYsjgLKLl6vU4pP4Vd0f4GSYyGOoCptNfwlg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/majaliwa-amwakilisha-rais-samia-katika.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/majaliwa-amwakilisha-rais-samia-katika.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy