WATU 22 wamefariki dunia huku zaidi ya 30 wakijeruhiwa katika ajali ya barabarani ikihusisha basi lenye namba za usajili T 732 ATH mali ya ...
WATU 22 wamefariki dunia huku zaidi ya 30 wakijeruhiwa katika ajali ya barabarani ikihusisha basi lenye namba za usajili T 732 ATH mali ya Kampuni ya AHMEED linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Tanga kugongana uso kwa uso na lori lenye namba IT 2816 eneo la Melea kibaoni barabara ya Iringa-Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim amesema, ajali hiyo imetolea Ijumaa Machi 18, 2022 saa 10 jioni wakati basi la Ahmed likitokea Mbeya kwenda Tanga kugongana na lori la lilikokuwa likisafiri kwenda nje ya nchi.
Amesema ajali imetokea wakati lori hilo likijaribu kumkwepa mwendesha pikipiki ndiyo likagongana na basi hilo, yakanasana na kusababisha vifo vya watu 13 papo hapo.
Credit: MPEKUZI
Thanks for your time please share with your friends
COMMENTS