Taasisi Zatakiwa Kuzingatia Sheria Ya Ununuzi Ya Umma
HomeHabari

Taasisi Zatakiwa Kuzingatia Sheria Ya Ununuzi Ya Umma

Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma Serikali imezielekeza Taasisi   zote nchini   kuzingatia matakwa ya Sheria ya   U nunuz...


Na. Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali imezielekeza Taasisi zote nchini kuzingatia matakwa ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2013 na umuhimu wake katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande, alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Eng. Mwanaisha Ng'azi Ulenge, aliyetakakujua wakati ambao Serikali itafanya tathmini kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Manunuzi wa Umma ya Mwaka 2013 katika Sehemu ya 64(2)(C) ya Kanuni ya 30 C kama ilivyofanyiwa Marekebisho.

Mhe. Chande alisema katika kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma, SURA 410 pamoja na kanuni zake, Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) hufanya tathmini ya ununuzi na kuchapisha taarifa ya tathmini hiyo kila mwaka.

“Matokeo ya tathmini ya mwaka 2020/21 kuhusu kutenga fedha za ununuzi asilimia 30 kwa makundi maalumu imeonesha kuwa, kati ya taasisi 86 zilizofanyiwa ukaguzi, taasisi mbili (2) zilitenga fedha hizo, taasisi tatu (3) zilitenga kiwango pungufu na taasisi 81 hazikutenga kabisa”, alibainisha Mhe. Chande.

Aidha, aliviagiza Vitengo vya Ukaguzi wa Ndani kuhakikisha kuwa Ripoti za kila Robo Mwaka ambazo huwasilishwa PPRA kuwa na taarifa kuhusu utekelezaji wa sheria katika eneo hilo.

Wakati huohuo, Mhe. Chande alisema katika mwaka 2021/22 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakamilisha tathmini ambayo itabainisha maeneo yenye uhitaji wa kujengwa ofisi za Mamlaka hiyo nchini kulingana na vigezo vilivyowekwa.

Alisema Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inautaratibu wa kupitia na kufanya tathmini kwa nchi nzima yenye lengo la kubaini maeneo yote yenye uhitaji wa kujengwa ofisi za TRA kwa ajili ya ufuatiliaji, usimamizi na ukusanyaji kodi ili kusogeza huduma za kikodi karibu na wananchi.

“Utaratibu huu unazingatia pamoja na mambo mengine, uwiano wa gharama za ukusanyaji wa mapato na kiwango cha kodi kinachotarajiwa kukusanywa wakati ofisi hizo zitakapofunguliwa kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi katika eneo husika”, alifafanua Mhe. Chande.

Alisema Serikali inadhamiria kuhakikisha kuwa maeneo yote ikiwemo Wilaya ya Mkalama yatakayokidhi vigezo stahiki yanajengwa ofisi za TRA



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Taasisi Zatakiwa Kuzingatia Sheria Ya Ununuzi Ya Umma
Taasisi Zatakiwa Kuzingatia Sheria Ya Ununuzi Ya Umma
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhU5wMs2_bIGHHhiVaJLVXJZONtCEBDqKyjsuHWxFYVt00ODlcGrMsm4zdeeTBTvcvCcEu4mAyJfkstKfcDpf9PbMhs9cohqMGahXvoK5PAqR7JEQBM3__JMklWgikdaR-Xdq9PZcgIfMEeaZyPkrs3Tefkbi1rjs7i293A2z04dxUK1f0XBXO-TD8ESw/s16000/1-6-scaled.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhU5wMs2_bIGHHhiVaJLVXJZONtCEBDqKyjsuHWxFYVt00ODlcGrMsm4zdeeTBTvcvCcEu4mAyJfkstKfcDpf9PbMhs9cohqMGahXvoK5PAqR7JEQBM3__JMklWgikdaR-Xdq9PZcgIfMEeaZyPkrs3Tefkbi1rjs7i293A2z04dxUK1f0XBXO-TD8ESw/s72-c/1-6-scaled.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/taasisi-zatakiwa-kuzingatia-sheria-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/taasisi-zatakiwa-kuzingatia-sheria-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy