Jeshi La Polisi Lakamata Jezi Feki, Watuhumiwa 15 Wakamatwa
HomeHabari

Jeshi La Polisi Lakamata Jezi Feki, Watuhumiwa 15 Wakamatwa

JESHI Jeshi la Polisi limekamata jezi feki  zinazouzwa zinazotumiwa na timu mbalimbali za hapa nchini. Akizungumza na waandishi wa haba...

Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ahimiza ufanisi uratibu wa shughuli za vijana na ajira
Wakulima wa miwa Kilombero wafunguka juu ya Sukari
Habari kubwa Magazetini Kenya leo August 1, 2024

JESHI Jeshi la Polisi limekamata jezi feki  zinazouzwa zinazotumiwa na timu mbalimbali za hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya Polisi, David A. Misime - SACP amesema utengenezaji na uuzaji wa jezi feki (zisizo na kiwango) ni kosa la jinai na kibaya zaidi wanaofanya hivyo wanakuwa ukwepaji kulipa kodi kwa sababu hazipitii katika mfumo ulio rasmi.

Misime - SACP amesema baadhi ya timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, huingia mikataba na kampuni mbalimbali ya kutengeneza jezi na pale zinapouzwa kiasi fulani huingia katika timu ili kugharamia mahitaji ya wachezaji kama mishahara.

Amesema Timu ya Polisi Tanzania imefanya hivyo kwa kuingia mkataba na baadhi ya kampuni kama vile Lodhia Group of Companies na Kampuni ya Vunja Bei.

Kwa bahati mbaya na kwa nia ovu ya kujipatia fedha kinyume cha sheria za nchi, baada ya timu hizo kuingia mikataba, utengenezaji, usambazaji na mauzo yanapo anza wapo watu wanaotengeneza jezi zilizo chini ya kiwango (jezi feki) kwa kutumia nembo zilezile na kuanza kuziuza mitaani. Kwa kufanya hivyo huinyima serikali mapato na kibaya zaidi timu hukosa fedha zikiwepo za kuwalipa wachezaji.

aAmesema  msako ulioendeshwa na Jeshi la Polisi watuhumiwa 15 wameshakamatwa kutoka maeneo ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Tabora na Tunduma ambapo jumla ya Jezi feki 279, Urembo (ribons) 300 na Kofia 6 zimekamatwa. Kesi zimefunguliwa dhidi yao na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha katika uchunguzi uliofanyika imebainika kuwepo na wafanyabiashara waliofanya mawasiliano na viwanda vya ndani na nje ambavyo jezi halali hutengenezwa wakitoa oda ya kutengenezewa jezi feki. Hawa nao ambao jumla yao ni 11 wamefunguliwa jalada, wamehojiwa na ushahidi unaendelea kukusanywa.

Amesema Jeshi la Polisi Tanzania linatoa wito kwa watu wanaofanya hivyo kuacha mara moja kwani watachukuliwa hatua endapo wataendelea kufanya uhalifu huo.

Aidha ametoa wito kwa timu ambazo zitabaini watu wanaotengeneza na kuuza jezi feki zenye nembo walizokubaliana katika mikataba walioingia na kampuni wasisite kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya watu hao.

Pia amewaasa Watanzania, wanapo nunua jezi za timu wanazozipenda na kuzishabikia, wanunue kwenye maduka stahiki na pale watakapo baini kuuziwa jezi feki wasisite kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi. Wananchi tunaomba watambue jezi hizo feki wanauziwa bei ile ile ya jezi halali, ambazo ukitumia hazidumu kama zile halali.

Tukumbuke tatizo la bidhaa bandia (feki) ni la dunia nzima, tukilifumbia macho hili la jezi feki wahalifu wana tabia ya kunogewa, watahamia hata katika dawa za kutibu binadamu, mifugo na hata katika vifaa mbalimbali vya matumizi ya binadamu na madhara yatakuwa kwetu sote.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Jeshi La Polisi Lakamata Jezi Feki, Watuhumiwa 15 Wakamatwa
Jeshi La Polisi Lakamata Jezi Feki, Watuhumiwa 15 Wakamatwa
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgBGHSWBBeOKfJDJjDLa7N9_bsGQ34-g9ch004G8zcqzNs-OfnUmwetkMzvnAt7bPYp_6XShk44TeUhdFKYOmUsZOS3tuXnx6JdXucCaMly_4B9jnAv6h_oLQUaJ5-Wk1Am8tNGYY1k8XpHTrUDSLyirCiGodUiW6m6vDOPXYjlejsQoiTz5FVPfkG4PQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgBGHSWBBeOKfJDJjDLa7N9_bsGQ34-g9ch004G8zcqzNs-OfnUmwetkMzvnAt7bPYp_6XShk44TeUhdFKYOmUsZOS3tuXnx6JdXucCaMly_4B9jnAv6h_oLQUaJ5-Wk1Am8tNGYY1k8XpHTrUDSLyirCiGodUiW6m6vDOPXYjlejsQoiTz5FVPfkG4PQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/jeshi-la-polisi-lakamata-jezi-feki.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/jeshi-la-polisi-lakamata-jezi-feki.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy