SERIKALI YAZUIA BASATA KUKAGUA NYIMBO ZA WASANII
HomeMichezo

SERIKALI YAZUIA BASATA KUKAGUA NYIMBO ZA WASANII

  SERIKALI imesitisha utekelezaji wa kanuni ya kukagua nyimbo za wasanii kabla hazijaenda kwa walaji.  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni...


 SERIKALI imesitisha utekelezaji wa kanuni ya kukagua nyimbo za wasanii kabla hazijaenda kwa walaji.

 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa ametoa uamuzi huo Mei 8, 2021 alipokutana na viongozi wa mashirikisho kujadili kuhusu kanuni hiyo iliyoibua mijadala mingi mitandaoni.

 

Bashungwa amesitisha utekelezaji wa kanuni hiyo mpya ya kugagua nyimbo za wasanii kabla hazijaenda kwa walaji, iliyoanza kukaziwa utekelezaji wake Mei mwaka huu na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

 

Baada ya kumalizika kwa kikao hicho kilichochukua takribani saa tatu, Waziri Bashungwa alieleza yaliyoafikiwa baada ya kupokea kwa maoni ya wadau na kueleza ameamua kusitisha utekelezaji wa kanuni hiyo.

 

“Baada ya kusitisha kanuni hii, kitakachofanyika ni Basata kukaa na wadau na kupokea maoni yao kuona namna gani bora ya kuja na kanuni za maadili ambazo hazitaumiza pande yoyote,” amesema Waziri Bashungwa.

 

Awali wasanii wakitoa maoni yao kuhusiana na kanuni hiyo,akiwemo Nikki Mbishi, amesema kanuni imetaja sanaa kwa ujumla, jambo ambalo litakuwa gumu katika utekelezaji.


“Sanaa ni uwanja mpana, kwa kanuni hii ni wazi kwamba hata nguo msanii atakayovaa inapaswa kwenda kukaguliwa kwanza na baraza kabla hajarekodi nyimbo au kupanda jukwaani,”.

 

Kwa upande wake Mwimbaji wa Taarabu, Mzee Yusufu ,amesema ipo haja ya Bongofleva kutengeneza kanuni zao kwa kuwa muziki wanaoufanya ni tofauti na ule wa dansi na taarabu.

 

Wakati Msanii Fid Q, amesema muziki kwa sasa ni biashara, hivyo unapouwekea mipaka ni kutaka kupoteza ubunifu na ushindani na wasanii wa ndani na nje ya nchi.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: SERIKALI YAZUIA BASATA KUKAGUA NYIMBO ZA WASANII
SERIKALI YAZUIA BASATA KUKAGUA NYIMBO ZA WASANII
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgQo28jCSqktRZ-akoPCVbtYEISAm2oJVN68bJlt8UmUpJBJt_TtIk3ebBo36DyNJoSR6YA-5hJ9XEgOUx6kHmJpW1VLETijHAVGGsTM2Ijk3Ytq6rDAbhck45i-6pmMSHJwncvnljiZAFw/w640-h426/BASHUNGWA.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgQo28jCSqktRZ-akoPCVbtYEISAm2oJVN68bJlt8UmUpJBJt_TtIk3ebBo36DyNJoSR6YA-5hJ9XEgOUx6kHmJpW1VLETijHAVGGsTM2Ijk3Ytq6rDAbhck45i-6pmMSHJwncvnljiZAFw/s72-w640-c-h426/BASHUNGWA.png
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/serikali-yazuia-basata-kukagua-nyimbo.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/05/serikali-yazuia-basata-kukagua-nyimbo.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy