HomeHabariTop Stories

Wakulima wa miwa Kilombero wafunguka juu ya Sukari

Wakulima wa Miwa katika Bonde la Mto Kilombero Mkoani Morogoro wamekanusha taarifa zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina na baadhi w...

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo July 2, 2024
Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ahimiza ufanisi uratibu wa shughuli za vijana na ajira
Habari kubwa Magazetini Kenya leo August 1, 2024

Wakulima wa Miwa katika Bonde la Mto Kilombero Mkoani Morogoro wamekanusha taarifa zilizotolewa na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina na baadhi watu waliodanganya kuwa ni wawakilishi wa wakulima na kudai bei ya miwa imeporomoka na hawalipwi fedha zao kwa wakati.

Wakizungumza na waandishi wa habari wilayani Kilombero viongozi wa umoja wa vyama vya wakulima pamoja na baadhi ya wakulima wanaounda vyama 17 vya ushirika (AMCOS), wamekanusha taarifa hizo wakidai kuwa ni uzushi na upotoshaji unaofanywa kwa maslahi ya kisiasa.

“Hakujawahi kutokea bei ya miwa kushuka kwani tangu tuanze kuuza miwa msimu huu tumeuza kwa bei ya laki moja na elfu nane (108,000) – tofauti na hizi taarifa za uongo zinazosambaa”

Aidha wakulima hao wamedai kuwa hakujawahi tutokea ucheleweshwaji wa muda mrefu wa malipo kwa wakulima kutoka kwenye kiwanda cha kuzalisha miwa na badala yake malipo yalichelewa kwa siku mbili tu kutokana na mifumo mipya iliyowekwa kiwandani hapo ambapo walitakiwa kulipwa tarehe 15 na badala yake walilipwa tarehe 17.

Wakulima hao wamesisitiza kwamba hakuna athari zozote zilizowapata kufuatia uamuzi wa serikali kutoa vibali vya kuagiza sukari nje kupunguza ongozeko la bei ya bidhaa hiyo ili kuleta ahueni kwa wananchi.

Vilevile wakulima hao wamesema kuwa vyama vyao vina ushirikiano mzuri na kiwanda cha sukari Kilombero na wanayo matumaini makubwa ya mageuzi ya zao hilo, kwa kuwa kiwanda hicho kinalenga kufanya upanuzi mkubwa utakaopelekea wakulima kuuza miwa kwa wingi zaidi.

The post Wakulima wa miwa Kilombero wafunguka juu ya Sukari first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/SKC8NID
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wakulima wa miwa Kilombero wafunguka juu ya Sukari
Wakulima wa miwa Kilombero wafunguka juu ya Sukari
https://i.ytimg.com/vi/ZCCGpQbd5a8/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/ZCCGpQbd5a8/default.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/wakulima-wa-miwa-kilombero-wafunguka.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/wakulima-wa-miwa-kilombero-wafunguka.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy