Na Saleh Ally UKIACHANA na suala la kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara nne mfululizo katika kipindi hiki, moja ya sifa kub...
Na Saleh Ally
UKIACHANA na suala la kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara nne mfululizo katika kipindi hiki, moja ya sifa kubwa kabisa ya Klabu ya Simba ni uongozi unaofuata weledi.
Simba ndio mfano wa uongozi kwa klabu nyingine, kwamba wanaendesha mambo yao kwa kufuata utaratibu sahihi kabisa kulingana na ubora wao.
Kweli kikosi chao ni bora, mambo yao yanaonekana yanakwenda kwa utaratibu mzuri kabisa katika kipimo sahihi na kila kitu ni kizuri.
Wengine wanapaswa kuanza kuiga au wameanza kuiga kutokana na wanavyosikia namna ambavyo Simba inaendeshwa. Kitu kizuri ni chachu ya mabadiliko na baadaye mafanikio kwa wengine.
Kwa sasa, mambo yanaanza kwenda tofauti na huenda ikaamka picha mpya kwamba inawezekana hata kwa watu wanaojitambua na kuendesha kazi zao kwa ufasaha kuanza kulumbana hadharani.
Kuna sauti ambayo imeanza kusambaa usiku wa kuamkia juzi, ikisikika Msemaji wa Simba, Haji Manara akimshutumu mambo kadhaa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.
Maneno ni mengi na inaonekana katika shutuma hizo, Manara analia kudharauliwa, kunyanyaswa na kufanyiwa roho mbaya huku akisisitiza kwamba atazungumza baada ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga kule Kigoma, Jumapili.
Manara ameendelea kueleza anavyokerwa na mambo kadhaa huku akitupa shutuma lukuki kwa Barbara ambaye ameendelea kuwa kimya.
Mchana kwenye ukurasa wake wa Instagram, ameeleza kwamba aliyevujisha sauti ile ni Barbara mwenyewe kwa kuwa yeye ndiye alimtumia. Akasisitiza aliamini anazungumza naye huku akiwa amejipanga kuzungumza baada ya mechi hiyo ya Kigoma, lakini sauti hiyo imevujishwa kwa makusudi.
Hilo ndiyo gumzo kubwa zaidi katika mchezo wa soka, wakati watu wanakwenda katika fainali ya Kombe la Shirikisho mjini Kigoma, sura imekuwa tofauti na sasa ni Manara wa Simba dhidi ya Barbara wa Simba. Jiulize!
Vipi iwe viongozi wa Simba walumbane katika kipindi kama hiki ambacho unatarajia kuiona timu hiyo ikijipanga vizuri kwa ajili ya kushinda mchezo huo?
Kati ya maneno aliyoyazungumza Manara ni kuhusiana na yeye kutuhumiwa kwenda kwenye kambi ya Yanga huku akisisitiza anadhalilishwa na bosi wake huyo ambaye amemuita ni anayependa umaarufu.
Yanga kwao wanaona ni kama hasira za mkizi au vita ya vifaranga vya kuku inayokwenda kuwa faida kwa kunguru au mwewe, jambo ambalo kwa Simba linawapitisha katika sifa mbovu kabisa.
Katika yale maneno, Manara mwisho
alimaliza kwa kumueleza bosi wake huyo
mwanamama “koma”. Lile neno
linalomsisitiza mtu kuacha au kuachana
na jambo fulani. Nami niwasisitize
kwamba iwe hadharani au chinichini,
bado wote hawakupaswa kuonyesheana
nani zaidi kwa kipindi hiki.
Tunamuona Barbara akiwa
amenyamaza, lakini kwa mujibu wa
Manara alimshambulia kwa maneno
kadhaa ambayo yanaonekana kumkera
na kuanzisha mjadala huo ambao binafsi
nauona hauna manufaa kwa Simba kwa
kuwa wao wote wawili ni waajiriwa wa
Simba hata kama ni kweli Barbara
alisema yeye ndiye mwenye Simba kama
alivyosema Manara. Kama viongozi ambacho walipaswa kukiangalia ni maslahi mapana ya kikosi
cha Simba na Wanasimba
wanaoizunguka klabu hiyo. Ikishinda ni
faraja kubwa sana kwao na ikipoteza ni
maumivu makubwa, sasa vipi waingize
jambo linalopoteza mwendo wao
unaopelekea umoja na mafanikio
ambayo yamewapa sifa.
Sifa ya weledi inapotea, sifa ya uongozi
bora kwao inapotea na hata lile jambo la
kushindwa kwamba wanapaswa
kulumbana wakati gani basi ni shida
nyingine kubwa na litakuwa jambo bora
wakikaa kimya, baadaye
wakakutanishwa na ikiwezekana
kuyaweka mambo sawa na waendelee.
Simba inaongozwa na watu ambao ndio
wawakilishi wa kikosi chao. Dhamana
waliyopewa ni kubwa sana, asiwepo
anayeona ni zaidi ya mwingine, asiwepo
atakayeona ni mkubwa kuliko klabu au
bora sana zaidi ya wengine. Ikiendelea
hivyo, watapoteza uelekeo na kuna siku,
watashangaa kuona walipo ni chini ya
wengine.
Kama kuna mgogoro, mazungumzo
hayajawahi kushindwa na kama ni chuki
za mioyo baina yao, basi kuna viongozi
wanaoweza kufanya wakayamaliza lakini
kwa kilichotokea, badala ya kuishia kwa
Manara au Barbara kinaiangusha Simba
yenyewe kuonekana imefeli kiuongozi.
Wote wawili mkome!
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS