Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ahimiza ufanisi uratibu wa shughuli za vijana na ajira
HomeHabariTop Stories

Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ahimiza ufanisi uratibu wa shughuli za vijana na ajira

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete amehimiza menejimenti na watumishi ...

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete amehimiza menejimenti na watumishi wa ofisi hiyo kuongeza ufanisi katika kuratibu shughuli za vijana na masuala ya ajira nchini ili kutimiza matarajio ya vijana katika kukuza maendeleo ya Taifa.

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema kuwa dhamira ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wanapata ajira zinazozalishwa na sekta mbalimbali nchini.

Amesema hayo leo Julai 31, 2024 wakati alipowasili kwenye hiyo Ofisi iliyopo Mji wa serikali Mtumba kwa mara ya kwanza baada ya kuapishwa Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai, 2024.

Vile vile Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema, Wananchi ambao kwa asilimia kubwa ni vijana wanatarajia makubwa kupitia wizara hiyo ambayo inasimamia maeneo mbalimbali ikiwemo masuala ya maendeleo ya Vijana, Ajira, ustawi wa Watu wenye Ulemavu, Wafanyakazi, Waajiri na Wastaafu.

“Matarajio yangu ni kuona tunawafikia vijana kwa wingi, kutambua changamoto zanazowakabili na kutatua changamoto hizo,” amesema Mhe. Ridhiwani

Kwa upande mwengine, Mhe. Ridhiwani Kikwete amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Waziri katika Ofisi hiyo na kuahidi kushirikiana na watumishi wa Ofisi yake ili kufanikisha malengo na mipango yaliyokusudiwa na Serikali katika kuwahudumia wananchi.

Waziri Ridhiwani Kikwete amewasili katika ofisi hiyo ambapo alipokelewa na Katibu Mkuu, Mhe. Mary Ngelela Maganga.

The post Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ahimiza ufanisi uratibu wa shughuli za vijana na ajira first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/em0Tftg
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ahimiza ufanisi uratibu wa shughuli za vijana na ajira
Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ahimiza ufanisi uratibu wa shughuli za vijana na ajira
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/08/4370ca38-116e-4969-b1aa-accd53b59ea4-950x633.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/mhe-ridhiwani-jakaya-kikwete-ahimiza.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/mhe-ridhiwani-jakaya-kikwete-ahimiza.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy