Dkt. Jafo Atoa Siku 45 Kukamilishwa Mradi Wa Maji
HomeHabari

Dkt. Jafo Atoa Siku 45 Kukamilishwa Mradi Wa Maji

Uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa umepewa siku Arobaini na tano kukamilisha usimikaji wa mabomba na matanki ya kuhifadhi maji safi na salama k...

Bajeti ya trilioni 14.94 Wizara ya fedha yapita
Mawakili waomba Sabaya akatibiwe uvimbe kichwani
Watumishi Wajengewa Uwezo Kuhusu Mradi Wa Tanzania Ya Kidijitali


Uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa umepewa siku Arobaini na tano kukamilisha usimikaji wa mabomba na matanki ya kuhifadhi maji safi na salama kwenye vijiji vya Mbugani, Ngh’ambi na Kiegea katika Wilaya ya Mpwapwa.

Agizo hilo limetolewa  Desemba 23, 2021 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua Utekelezaji wa Mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia mifumo ikolojia vijijini ulipo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais na unatekelezwa katika Wilaya tano nchini ambazo ni Mpwapwa, Mvomero, Kishapu, Simanjiro na Kaskazini – A

Akiwa Wilayani Mpwapwa katika kijiji cha Nghambi Dkt. Jafo amekasirishwa na kitendo cha mkandarasi wa Kampuni ya Make  Engineering  kutoka Dar es Salaam kutokamilisha kwa wakati mradi wa uchimbaji wa visima vyenye urefu wa mita 150 na kumuagiza mkandarasi huyo kukamilisha kazi mapema iwezekanavyo.

Amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha huduma zinasogezwa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

“Natoa siku Arobaini na tano tu maji yaanze kutoka hapa, mradi huu ukamilike. Wananchi hawa wanataka maji mapema, hakuna kwenda sikukuu na watumishi acheni kukaa maofisini, simamieni hili kikamilifu” Alisisitiza Dkt. Jafo.

Aidha, ametoa rai kwa wakazi wa Mbugani, Ngh’ambi na Kiegea kutumia vizuri mvua zinazonyesha kwa kupanda miti kwa vingi ili kulinda mazingira, na kusisitiza kuwa agenda ya mazingira ndio kipaumbe cha Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Bw. Josephat Maganga amesema atahakisha ndani ya siku arobaini na tano kazi zote zinakamilika na huduma ya maji inatolewa kwa wananchi.

Mradi wa kuhimili badiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini unafadhiliwa na Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi kwa Nchi Maskini  kupitia Mfuko wa Dunia wa Mazingira ambapo kuna shughuli za uchimbaji wa visima, ujenzi wa josho, uchimbaji wa lambo na utengenezaji wa majiko banifu. Miradi yenye jumla ya Tshs. 2,257,042,400/- imeidhinishwa kutekelezwa katika Wilaya ya Mpwapwa.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt. Jafo Atoa Siku 45 Kukamilishwa Mradi Wa Maji
Dkt. Jafo Atoa Siku 45 Kukamilishwa Mradi Wa Maji
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgNSTWYeXnhbNWxFuHwpLhRS6K7pz98v-bz4baFsXo4ZITXObYp8ypUqCRfc9gQ4I-Boe-IJhdYmdMI0UJG1JaaZSCfATn4BDyvqd--tDYSKFVi1_l9WsBLa1s90PL1aE6y6jWR35ic_GelnL3Z6HdmHtStNykeTkuZIuY6zJ25zPicZWSPfHyvDItMVQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgNSTWYeXnhbNWxFuHwpLhRS6K7pz98v-bz4baFsXo4ZITXObYp8ypUqCRfc9gQ4I-Boe-IJhdYmdMI0UJG1JaaZSCfATn4BDyvqd--tDYSKFVi1_l9WsBLa1s90PL1aE6y6jWR35ic_GelnL3Z6HdmHtStNykeTkuZIuY6zJ25zPicZWSPfHyvDItMVQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/dkt-jafo-atoa-siku-45-kukamilishwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/dkt-jafo-atoa-siku-45-kukamilishwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy