ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi leo Machi 19, 2021 kuwa Rais wa ...
ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi leo Machi 19, 2021 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hafla hiyo imefanyika katika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo uapisho huo umehudhuriwa na viongozi waandamizi wa Serikali, Majeshi ya Ulinzi pamoja na marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uapisho huo unakuja kwa mujibu wa katiba yay a Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar kwa maradhi ya moyo.
Mama Samia anakuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS