HomeHabariTop Stories

CCM yawaonya wenyeviti watakaotumia madaraka yao kuumiza wananchi

Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe kimewataka wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji waliochaguliwa kwenda kusimamia shughuli za mae...

Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe kimewataka wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji waliochaguliwa kwenda kusimamia shughuli za maendeleo na miradi inayoendelea kwenye maeneo yao kwa kufuata utaratibu,sheria na kanuni zilipo ili kufanikisha maendeleo kwenye jamii zao kuliko kutumia nafasi walizopata kujinufaisha na kuwanyanyasa wananchi.

Agizo hilo limetolewa na katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Njombe Josaya Luoga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake baada ya mchakato wa uchaguzi kukamilika ambapo amesema Chama hicho hakitoi maelekezo kwa wenyeviti kwenda kutoza fedha kwa ajili ya mhuri kwa wananchi badala yake wakatoe huduma huku akitoa tahadhari kuwa wasidhani wanakwenda kupata fedha kwa kuwa kazi hiyo ni ya kujitolea.

“Kazi ya uenyekiti wa kijiji,kitongoji au mtaa ni ya kujitolea sasa isiende kutumika kama ndio kazi mama kwa hiyo tunawaomba wakatumie nafasi zao vizuri kutatua kero za wananchi badala ya kutumia nafasi hizo kuwaumiza wananchi na kujipatia vipato visivyo halali kwa kuwa kwa utaratibu wetu unapoomba nafasi yoyote ndani ya Chama chetu ambayo ni ya kujitolea ni lazima ueleze kazi yako mama,sisi tunaamini tumepata viongozi wenye sifa ya kuwatumikia wananchi”amesema Luoga

Amesema katika uchaguzi uliofanyika Novemba 27 Chama hicho mkoa wa Njombe kimepata ushindi wa zaidi ya asilimia 99.7% ambapo katika vijiji 381 vya mkoa huo CCM imepata ushidi kwa kushinda vijiji 377 na katika mitaa 82 Chama hicho kimeshinda mitaa 81 na katika vitongoji 1832 wameweza kupata ushindi katika vitongoji 1819 huku kati ya wajumbe 3710 wakifanikiwa kupata 3698 ambapo amewashukuru wananchi na wanachama kwa kujenga imani kwa Chama hicho.

The post CCM yawaonya wenyeviti watakaotumia madaraka yao kuumiza wananchi first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/YopI0Cy
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: CCM yawaonya wenyeviti watakaotumia madaraka yao kuumiza wananchi
CCM yawaonya wenyeviti watakaotumia madaraka yao kuumiza wananchi
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/11/ccm-yawaonya-wenyeviti-watakaotumia.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/11/ccm-yawaonya-wenyeviti-watakaotumia.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy