Wizara yanishati yakabidhi gari la kubebea nguzo za umeme Mbinga
HomeHabariTop Stories

Wizara yanishati yakabidhi gari la kubebea nguzo za umeme Mbinga

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Julai 20, 2024 amekabidhi gari la kubebea nguzo katika Ofisi ya TANESCO Wilaya ya Mbinga mkoan...

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Julai 20, 2024 amekabidhi gari la kubebea nguzo katika Ofisi ya TANESCO Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Wakati akikabidhi gari hilo Mhe. Kapinga amesema Serikali itaendelea kuboresha maslahi, vitendea kazi na mazingira ya kazi kwa Wafanyakazi wa TANESCO ili kuwapa motisha ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii.

“Kulikuwa na changamoto ya kubeba nguzo kupeleka kwenye maeneo mnayofanyia kazi, Serikali inaamini magari haya yataleta tija na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi ikiwemo kutoa huduma kwa wakati kwa wateja.” Amesema Kapinga

Akizungumzia changamoto ya kukatika kwa umeme wilayani Mbinga, Kapinga amesema Serikali imeshaweka mikakati ya kujenga kituo kipya cha umeme ambacho kitaboresha hali ya upatikaji umeme.

Ameongeza kuwa, kituo hicho cha kupokea na kupoza umeme kitajengwa katika mradi wa Gridi Imara Awamu ya Pili.

Amesema TANESCO inaendelea kuboresha miundombinu ya umeme wilayani humo wakati ujenzi wa kituo cha kupokea na kusambaza umeme ukisubiriwa.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kapinga amewahakikishia wananchi kuwa, Wizara ya Nishati chini ya uongozi wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, itaendelea kuboresha utoaji wa huduma na upatikanaji wa nishati ya umeme nchini.

Awali, Meneja wa TANESCO Wilaya ya Mbinga, Mhandisi Edward Kweka alisema kuwa walikuwa wakikutana na changamoto ya ubebaji nguzo kutokana na kutokuwepo kwa gari la kubebea nguzo hizo..

Mhandisi Kweka amesema gari hilo litawasaidia kutoa huduma kwa ufanisi na kuahidi kulitunza.

TANESCO Wilaya ya Mbinga inajumla ya wateja 37,925 na inapokea umeme wa gridi ya Taifa wa kilovoti 33 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Songea.

The post Wizara yanishati yakabidhi gari la kubebea nguzo za umeme Mbinga first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/S21Msgp
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wizara yanishati yakabidhi gari la kubebea nguzo za umeme Mbinga
Wizara yanishati yakabidhi gari la kubebea nguzo za umeme Mbinga
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/07/20a02f3f-f2c8-496d-907f-0de386a5c930-950x581.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/07/wizara-yanishati-yakabidhi-gari-la.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/07/wizara-yanishati-yakabidhi-gari-la.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy