ANTHONY Martial, amejikuta akiingia katika wakati mgumu kwa mara nyingine baada ya kushambuliwa mitandaoni wakati timu yake ya Manches...
ANTHONY Martial, amejikuta akiingia katika
wakati mgumu kwa mara nyingine baada ya
kushambuliwa mitandaoni wakati timu yake ya
Manchester United ikipata sare ya bao 1-1 dhidi
ya West Bromwich Albion, juzi Jumapili.
Mfaransa huyo alianza katika kikosi cha
kwanza kabla ya kutolewa katika dakika ya 66
baada ya timu yake kushindwa kuonesha
makali ya kufunga ili kuwafukuzia kwa ukaribu
wapinzani wao, Man City ambao wanaongoza
katika msimamo wa Premier League.
Mara baada ya mechi hiyo kumalizika, kulianza
kusambaa meseji za ujumbe wa chuki na
nyingine za ubaguzi wa rangi zikiwa na alama
au picha mbalimbali zinazoonesha ubaguzi
kupitia Mtandao wa Instagram.
Hii ni mara ya pili kwa mshambuliaji huyo
kushambuliwa hivi karibuni tangu kuanza kwa
mwaka huu, mara ya kwanza ilikuwa baada ya
United kufungwa 2-1 na Sheffield United.
Wachezaji wengine wa Premier League ambao
wamewahi kuhusika katika kushambuliwa kwa
maneno kama ilivyo kwa Martial ni Reece
James na Antonio Rudiger wa Chelsea na
Romaine Sawyers wa West Brom.
Kumekuwa na presha nyingi juu ya watu
wanaohusika kutoa kauli za kibaguzi
mitandaoni, wadau wa soka wakiwemo
wachezaji wakitaka mitandao husika iwafichue
na ikiwezekana iwafungie lakini haijawa hivyo.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS