Tiwa Savage akiongea na wanafunzi nchini Uganda Nyota wa kike wa muziki wa Nigeria Tiwa Savage amebainisha matatizo ya ngono za mapema zil...
Tiwa Savage akiongea na wanafunzi nchini Uganda
Nyota wa kike wa muziki wa Nigeria Tiwa Savage amebainisha matatizo ya ngono za mapema zilivyoathiri maisha yake.
Mama kijacho huyo alibainisha matatizo ya ngono hizo wakati alipokuwa akiongea na wanafunzi wa shule ya Mariam High School ya jijini Kampala nchini Uganda.
Mwanamuziki huyo alisema kwasasa anatumia uzoefu wa maisha yake kutolea mfano kwa wasichana wadogo ambao anawaonea huruma kubeba mimba wakiwa na umri mdogo.
Tiwa alisema kuwa wakati yeye anasoma alikuwa anapenda kuimba ingawa wazazi wake walikuwa wanamsisitiza kusoma kwanza kabla ya kujiingiza kwenye muziki maana walikuwa wanapenda awe mwanasheria,injinia au daktari.
Aliongeza kuwa alipomaliza kupata degree ya kwanza ya biashara wazazi wake walimsisitiza tena ajiunge na chuo kikuu lakini yeye alikataa na kuwambia wazazi wake kuwa endapo atarudi chuo kikuu basi atachukua degree ya pili ambayo itakuwa niya muziki.
COMMENTS