Binti, Pendo Emmanuelle Nundi ametoweka tangu mwisho wa Desemba. Polisi wa Tanzania wametoa ofa ya zawadi kwa taarifa itakayopeleke...
Pendo Emmanuelle Nundi, 4, alitekwa nyara mwezi uliopita. Baba wa mtoto huyo ni mmoja wa watu 15 ambao watakamatwa kwa kutoweka kwake.
Viungo vya albino, ambao wamekosa rangi fulani katika ngozi yao, vinatafutwa na waganga wa jadi.
Tanzania iliwafungia waganga wa jadi mwezi uliopita ili kuzuia mashambulizi dhidi ya albino.
Polisi wanatoa ofa ya milioni tatu za Kitanzania (dola 1,700; pauni 1,100) kusaidia kumpata binti aliyetoweka awe “hai au amekufa”.
Wajomba wawili wa binti huyo wameshakamatwa kama sehemu ya uchunguzi.
Kuna zaidi ya watu 33,000 nchini Tanzania wanaoamiki kuwa na ulemavu wa ngozi.
Albino wapatao 70 wameshauawa tangu mwaka 2000 lakini ni watu wachache walioshtakiwa kwa mauaji.
COMMENTS