Timu zinazoshiriki michuano ya kombe la Afrika toka kundi A ni Congo, Gabon na Burkina Faso na wenyeji Equatorial Guinea zinatofautiana ...
Equatorial Guinea ikiwa imeorodheshwa nambari 181 katika orodha ya Fifa, ndio mwenyeji wa michuano hii.
Gabon haikupoteza katika michuano ya kufuzu lakini ilishinda mchezo mmoja tu katika michuano iliyochezwa ugenini maana kwamba timu huyo itamtegemea sana mshambuliaji wake Pierre-Emerick Aubameyang ambae atakua na mzigo wa kuibeba timu hiyo.
Wakiwa wanajulikana kwa jina la utani Mashetani wekundu, Congo ndio wageni sana wa hivi karibuni katika michuano hio. Kocha wao ni Wily Claude LeRoy anaweza kuwawezesha kufanya vizuri hasa baada ya kuwabandua mabingwa Nigeria katika michuano ya kufuzu.
Wenyeji Equatorial Guinea walifanikiwa kufika robo fainali kwenye michuano iliyopita na mashabiki wao wana matumaini kwamba watafika mbali sababu wao ndiyo wenyeji.
COMMENTS