Leo ndo leo, mbabe kujulikana
HomeMichezoKitaifa

Leo ndo leo, mbabe kujulikana

Pambano la Nani Mtani Jembe la leo litakuwa ni la pili baada ya lile lililofanyika mwaka jana kwenye uwanja huo wa taifa Dar es Salaam n...

JK aonya wahujumu wa Katiba mpya
Wamiliki wa mabasi wacharukia nauli
MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MKOA WA DAR ES SALAAM YAZINDULIWA RASMI,WANANCHI WATAKIWA KULINDA NA KUTUNZA MIUNDOMBINU.‏


Pambano la Nani Mtani Jembe la leo litakuwa ni la pili baada ya lile lililofanyika mwaka jana kwenye uwanja huo wa taifa Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1

KLABU za soka za Simba na Yanga leo  zinatarajia kuchuana kuwania milioni 100 ukiwa ni mchezo maalumu ulioandaliwa na wadhamini wakuu wa timu hizo Kampuni ya Bia ya Kilimanjaro uliopewa jina la Nani Mtani Jembe.




Pambano la Nani Mtani Jembe la leo litakuwa ni la pili baada ya lile lililofanyika mwaka jana kwenye uwanja huo wa taifa Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Matokeo ya mwaka jana ndiyo yatakayo changia mchezo wa leo kuwa na upinzani mkali kupita maelezo kwasababu ni wazi Yanga hawatokubali kupoteza mchezo huo kwa mara ya pili na kuwaachia wapinzani wao Simba kutamba,Lakini hata wapinzani wao Simba nao hawatokubali kuona rekodi yao ikivunja zaidi ya kupambana ili kuzidi kujiwekea rekodi.
Matokeo ya nje ya uwanja ambayo yanawahusisha mashabiki wa timu hizo mbili kwa kunywa bia ya Kilimanjaro yanaonyesha Yanga inaongoza kwa kujizolea asilimia kubwa ya pesa ambayo atapewa mshindi atakaye shinda uwanjani siku hiyo lakini hilo siyo la kujivunia sana zaidi ya ushindi ule wa uwanjani ambao ndio wenye hamasa kubwa kwa mashabiki wa timu hizo.
Timu hizo zitaingia uwanja wa taifa kesho kila moja ikiwa na matumaini ya kushinda mchezo huo kutokana na maandalizi ambayo zimeyafanya ikiwemo kuviboresha vikosi vyao kwa kusajili wachezaji wapya katika dirisha dogo .

Match Preview: Tanzania Prisons – Simba, wana msimbazi kuzindukia ugenini


Kwa upande wa Simba wamemsajili mfungaji bora wa Ligi ya Kenya aliyekuwa anachezea Gor Mahia Mganda Dan Sserunkuma na beki wa kulia wa Mtibwa Sugar Hassan Ramadhani huku kukiwa na tetesi kuwa inampango wa kuendelea na zoezi la usajili kwa kusajili beki kutoka Uganda.
Usajili huo umewapa tambo viongozi wa Simba pamoja na mashabiki wao na kuwa na matumaini makubwa ya kushinda pambano hilo wakijivunia Sserunkuma kuwa lazima atawafunga Yanga na kumaliza ukame wa mabao ambao ulikuwa ukiiandama timu hiyo kwenye mechi za Ligi.
Simba inaingia kwenye mchezo hui ikitokea Zanzibar lakini rekodi za hivi karibuni zinaonyesha Zanzibar siyo pazuri kwa timu hiyo kutokana na timu hiyo kuwa na matokeo mabaya kwenye ligi ya msimu huu kwa kucheza mechi saba na kushinda moja huku ikitoka sare mechi sita na iliweka kambi huko kabla ya ligi kuanza kitua ambacho kiliwalazimi viongozi hao kubadili makao na kuipeleka timu hiyo Afrika Kusini ilipokuwa inajiandaa kucheza na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Oktoba 18 msimu huu na timu hizo kutoka sare ya 0-0.
Usajili huo pia umempa matumaini makubwa kocha Patrick Phiri, ambaye kwa sasa ameanza kufikiria ubingwa baada ya kuwanyakua nyota hao na kuwabeza waza wapinzani wao kuwa lazima watafunga kutokana na safu kali ya ushambuliaji itakayokuwa inaongozwa na Waganda wawili Sserunkuma na Emmanuel Okwi ,ambaye mechi ya Nani Mtani Jembe ya mwaka jana alichezea Yanga na ndiye aliyefunga bao hilo moja.
Nayo Yanga imezidi kujipa matumaini ya kushinda pambano la kesho kutokana na uimara walichonacho ukilinganisha na kile cha wapinzani wao Simba.
Lengo la asilimia kubwa ya mashabiki wa Yanga ni kuiona timu yao inapata ushindi wa idadi kubwa ya mabao ili waweze kulipa kisasi cha mabao 5-0 waliofungwa na Simba misimu mitatu iliyopita lakini pia kulipa kisasi cha kipigo cha Nani Mtani Jembe iliyopita cha mabao 3-1.
Mwenendo wa Yanga inayoshika nafasi ya pili kwenye ligi ni tofauti kabisa na ule wa Simba Yanga imeshinda mechi nne za ligi ikatoka sare mchezo mmoja na kufungwa mbili mapungufu yake ni kuondokewa na mshambuliaji wake Mbrazili Geilson Santana Santos JAJA aliyeshindwa kurdi Tanzania kutokana na matatizo ya familia.
Lakini timu hiyo imeonekana kulitumia vizuri dirisha dogo la usajili kwa kumsajili Danny Mrwanda na kiungo Mbrazili Emerson de Olivier Roque na wakati wowote inaweza kusajili mshambuliaji mwingine raia wa Liberia Khap Sean Sherman ambaye huenda akavaa jezi za Yanga kesho kutokana na kufuzu vipimo vya afya.
Mbali na kutaka ushindi lakini kocha Marcio Maximo, anajua umuhimu way eye kushinda mchezo huo utamfanya awe na nafasi kubwa ya kuendelea kuaminiwa kuwa kocha wa Yanga kwani alipoteza imani kwa viongozi wa timu hiyo na mashabiki kwa kushindwa kuifunga Simba katika mchezo wa ligi kuu huku wapinzani wao wakiwa na mapungufu mengi ukilinganisha na kikosi alichokuwa nacho yeye.
Yanga yenyewe imepiga kambi katika Hotel ya LandMark iliyopo Boko nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na Maxomo ametamba kumtumia Mrwanda anayeogopewa sana na kocha wa Simba Patrick Phiri kutokana na uwezo wake atakaye cheza sambamba na Jerson Tegete mchezaji mwenye bahati kubwa ya kuifunga Simba.
Ushindani mkubwa katika mchezo wa kesho unatarajiwa kuonekana katika safu za ushambuliaji za timu zote mbili ambazo zimeongezwa wachezaji wapya katika dirisha dogo Sserunkuma atakuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa Simba huku Mrwanda na Sherman kama atakamilisha taratibu za usajili na Maximo kumpa nafasi naye atakuwa burudani tosha kwa mashabiki wa Yanga akiletwa kama mbadala wa JAJA.
Tusubiri dakika 90 za mchezo huo ili kuona upande gani utakuwa umefaidika na usajili ulioufanya katika dirisha dogo lakini pia ni kocha gani kati Phiri raia wa Zambia na Mbrazili Maximo ataweza kutoka uwanjani akiwa anacheka na kukumbatiana na wachezaji na viongozi wa timu yake.
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Leo ndo leo, mbabe kujulikana
Leo ndo leo, mbabe kujulikana
http://static.goal.com/392000/392003_heroa.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2014/12/leo-ndo-leo-mbabe-kujulikana.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2014/12/leo-ndo-leo-mbabe-kujulikana.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy