Wapiga kura Wapya 431,016 kuandikishwa Mkoa wa Tanga na Pwani
HomeHabariTop Stories

Wapiga kura Wapya 431,016 kuandikishwa Mkoa wa Tanga na Pwani

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Rufani Mhe. Jacobs Mwambegele, amefungua mkutano wa siku moja na wadau wa uchag...

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Rufani Mhe. Jacobs Mwambegele, amefungua mkutano wa siku moja na wadau wa uchaguzi mkoani Tanga leo, Februari 1, 2025. Mkutano huu ni sehemu ya maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa mikoa ya Pwani na Tanga, ambalo litafanyika kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025.

Zoezi hili litahusisha Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe, pamoja na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto, na Muheza. Katika kipindi hiki cha siku saba, inatarajiwa kuwa wapiga kura wapya 431,016 wataandikishwa, na hivyo kufanya jumla ya wapiga kura katika mikoa hiyo kufikia 2,727,318 baada ya zoezi kukamilika.

Mhe. Mwambegele amesisitiza umuhimu wa wadau wa uchaguzi kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa. Ameeleza kuwa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni hatua muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki.

Aidha, Tume imejipanga vizuri kwa ajili ya zoezi hili kwa kununua vifaa vipya vya BVR (Biometric Voter Registration) 6,000 ambavyo ni rahisi kubeba na vitasaidia kurahisisha zoezi la uboreshaji, hasa katika maeneo ya vijijini ambapo watendaji hulazimika kubeba vifaa kwa umbali mrefu.

Pia Tume inatoa wito kwa wananchi wote wenye sifa za kupiga kura katika mikoa ya Pwani na Tanga kujitokeza kwa wingi katika vituo vya uandikishaji ili kujiandikisha na kuboresha taarifa zao. Pia, inawahimiza wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini, asasi za kiraia, na vyama vya siasa, kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa zoezi hili.

Aidha wadau walioshiriki ambao ni vyama vya siasa,asasi za kiraia,wawakilishi wa wanawake,viongozi wa dini ,wawakilishi wa vijana na wazee wa kimila walishiriki katika mkutano wa Tume na wadau wa Uchaguzi na kutoa Maoni yao.
Kwa taarifa zaidi na ratiba ya uboreshaji kwa mikoa mingine, wananchi wanashauriwa kutembelea tovuti rasmi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi:

The post Wapiga kura Wapya 431,016 kuandikishwa Mkoa wa Tanga na Pwani first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/tfT4021
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wapiga kura Wapya 431,016 kuandikishwa Mkoa wa Tanga na Pwani
Wapiga kura Wapya 431,016 kuandikishwa Mkoa wa Tanga na Pwani
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250201-WA0014-1-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/wapiga-kura-wapya-431016-kuandikishwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/wapiga-kura-wapya-431016-kuandikishwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy