Naibu Katibu mkuu wizara ya madini asisitiza uwajibikaji weledi na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu
HomeHabariTop Stories

Naibu Katibu mkuu wizara ya madini asisitiza uwajibikaji weledi na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu

Baraza la Wafanyakazi ni chombo pekee kinachoweza kuunganisha Menejimenti na Wafanyakazi kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu...

Baraza la Wafanyakazi ni chombo pekee kinachoweza kuunganisha Menejimenti na Wafanyakazi kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Taasisi ambalo lipo kwa mujibu wa Agizo la Rais Na. 1 la Mwaka 1970 ambalo lina lengo la kuwashirikisha wafanyakazi wa ngazi zote.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kilichofanyika Mkoani Morogoro.

Aidha, Mbibo amewataka Wajumbe wa Baraza hilo na Watumishi wote wa GST kila mmoja wao kutimiza wajibu wake katika nafasi yake kwa weledi, ubunifu, uaminifu na ufanisi ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Naelewa kuwa Taasisi inatekeleza majukumu muhimu sana ya kutoa huduma za za tafiti za jiosayansi Jiolojia na Utafiti wa Madini kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini na wananchi kwa lengo la kubaini aina za miamba na madini inayopatikana nchini. Aidha, taasisi hii mdau mkubwa katika kufikia lengo la maono ya 2030 (Vision 2030). Hivyo kupitia baraza hili viongozi wanatakiwa kupata mawazo mapya ya kuboresha utendaji kazi” amesema Mbibo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa GST ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Mussa Budeba amemshukuru Mbibo kwa kushiriki na kulifungua Baraza hilo ambapo ameahidi kuyatekeleza yale yote yaliyoelekezwa na mgeni rasmi na pia amewataka Wajumbe wa Baraza hilo kutoa maoni na michango yao kwa uhuru na uwazi ili kuboresha utendaji kazi wa taasisi.

“Ninaamini wawakilishi wa wafanyakazi katika Baraza hili watapata fursa ya kuchangia mawazo yenye tija yatakayoleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Taasisi na kujenga uelewa wa pamoja wa majukumu yenu katika Baraza na kufanya Baraza kuwa sehemu nzuri ya majadiliano kwa ustawi wa Taasisi na Sekta kwa ujumla,” amesema Dkt. Budeba amesema.

Naye, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa GST Desideria Mgombezi amemshukuru Mbibo kwa kufungua kikao hicho ambapo ameahidi kuyafanyia kazi kwa weledi, uaminifu na ufanisi mkubwa yale yote yaliyoelekezwa na mgeni rasmi.

Pia, Katibu Msaidizi wa Baraza hilo Osiah Kajala ambaye pia ni Mchumi Mkuu wa GST amesema lengo la Baraza hilo ni kujadili utekelezaji wa bajeti iliyopita na kupitisha mpango wa bajeti kwa mwaka 2025/2026 kwa kuwahusisha wawakilishi wa Wafanyakazi ili kuongeza ufanisi, uhuru na uwazi pamoja na kujadili masuala mbalimbali hususan maslahi ya Watumishi.

Pia, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Taifa Straton Lufyagila amesema Baraza la Wafanyakazi lipo kwa mujibu wa Sheria ambapo wawakirishi wa Watumishi wa GST watapata fursa ya kutoa maoni kwa lengo la kuboresha ufanisi wa taasisi na kuongeza uwajibikaji wa Watumishi.

 

The post Naibu Katibu mkuu wizara ya madini asisitiza uwajibikaji weledi na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/8frWi4O
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Naibu Katibu mkuu wizara ya madini asisitiza uwajibikaji weledi na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu
Naibu Katibu mkuu wizara ya madini asisitiza uwajibikaji weledi na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250221-WA0058-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/naibu-katibu-mkuu-wizara-ya-madini.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/naibu-katibu-mkuu-wizara-ya-madini.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy