Hospitali ya rufaa Bombo Tanga kuwa na muonekano mpya
HomeHabariTop Stories

Hospitali ya rufaa Bombo Tanga kuwa na muonekano mpya

Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuanza ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo) kwa kuanzia na jengo la...

Picha mbalimbali za Uzinduzi wa Treni mpya ya kisasa SGR
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo July 2, 2024
Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete ahimiza ufanisi uratibu wa shughuli za vijana na ajira

Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuanza ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo) kwa kuanzia na jengo la wodi ya mama na mtoto kabla ya mwezi Mei mwaka huu, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za uzazi mama na mtoto na kuwa katika muonekano mpya.

Kauli hiyo imetolewa na Mhe. Jenista Mhagama jana Februari 22, 2025 alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tanga (Bombo) ambapo ametumia fursa hiyo kuihamasisha jamii ya mkoa huo kujitokeza kumpokea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa ziara yake mkoani humo.

“Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeipa kipaumbele Sekta ya Afya ambapo zaidi ya Shilingi Trilioni 8 zimewekezwa kwa kipindi hiki kifupi, ukiwemo mkoa wa Tanga,” amesema Waziri Mhagama.

Amesema kwa sasa Serikali inafanyia kazi changamoto ya majengo katika hospitali ya Bombo ambapo kwa ujenzi utaanza kwa kubadilisha muonekano wa hospitali hiyo na kuanza na jengo ya wodi wazazi ambalo litakuwa na huduma zote fungamanishi ikiwemo upasuaji pamoja na vipimo vya maabara.

“Kiu ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona tunaendelea kupunguza vifo vya mama na mtoto, kutoka vifo 556 kwa vizazi hai 100,000 hadi vifo 104 kwa vizazi hai 100,000, pia tungetamani hospitali yetu ya Bombo iendelee kuongoza kwenye zoezi la kuondoa vifo vya kina mama wakati wa kujifungua,” amesema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama ametumia wasaa huo kuihamasisha jamii ya watu wa mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwakuwa ameonesha uwezo wa kusimamia miundombinu ya utoaji wa huduma za afya.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Tanga (Bombo) Dkt. Frank Shega ameomba kuwezeshwa kifedha ili kukarabati majengo ya hospitali hiyo pamoja na kujenga majengo mengine mapya kwa ajili ya kuongeza huduma na kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa huduma za afya kwa wananchi.

The post Hospitali ya rufaa Bombo Tanga kuwa na muonekano mpya first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/jtS5zK7
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Hospitali ya rufaa Bombo Tanga kuwa na muonekano mpya
Hospitali ya rufaa Bombo Tanga kuwa na muonekano mpya
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250223-WA0021-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/hospitali-ya-rufaa-bombo-tanga-kuwa-na.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/02/hospitali-ya-rufaa-bombo-tanga-kuwa-na.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy