SIMBA YAIPOTEZA YANGA, AZAM FC KWENYE REKODI
HomeMichezo

SIMBA YAIPOTEZA YANGA, AZAM FC KWENYE REKODI

MSIMU wa 2020/21 kikosi cha Simba ambacho kimetwaa taji la Ligi Kuu Bara umeonekana kuwa bora kwao kwa kutawala katika takwimu nzuri. Si...


MSIMU wa 2020/21 kikosi cha Simba ambacho kimetwaa taji la Ligi Kuu Bara umeonekana kuwa bora kwao kwa kutawala katika takwimu nzuri.


Simba, licha ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu, ikiwa ni mara ya nne mfululizo lakini imeendelea kuonyesha kuwa ilikuwa ni timu tishio mara baada ya kufanya vizuri katika idara mbalimbali ndani ya uwanja na kuweka rekodi.

Simba katika ligi kuu msimu huu imefunga mabao 78 Yanga iliyo nafasi ya pili imefunga jumla ya mabao 52 na Azam FC iliyo nafasi ya tatu imefunga mabao 50.


Hii inatokana na wachezaji wa Simba binafsi kuonyesha viwango bora na kuwa na takwimu

nyingi bora kuwazidi wapinzani wao Yanga

pamoja na Azam FC.


Tukianzia katika orodha ya ufungaji bora wa ligi

kuu msimu huu, Simba ndio inaongoza kwa

kuwa na washambuliaji bora ambapo John

Bocco ana mabao 16, Chris Mugalu mabao 15 na Meddie Kagere mabao 13.


Ni Prince Dube pekee kutoka katika klabu ya Azam FC mwenye mabao 14 ambaye ameweza kuwatingisha washambuliaji wa Simba, jambo ambalo linamfanya kuwa mmoja kati ya washambuliaji bora waliofanya vizuri msimu huu.


Rekodi hiyo imewekwa na wachezaji wa Simba

pekee ya kuwa na washambuliaji watatu

waliofunga mabao 10 na kuendelea na hakuna

timu nyingine iliyofanya hivyo hata kwa upande wa Yanga na Azam ambazo ndio zimekuwa zikionyesha upinzani mkubwa zaidi kwa Simba.



Pia Simba imeonekana kuendelea kuwa bora mara baada ya kiungo wake Clatous Chama kuongoza katika orodha ya wachezaji waliotoa pasi nyingi za mabao ‘asisti’ akiwa ametoa jumla ya pasi 15 za mabao huku akifuatiwa na Luis Miquissone ambaye pia amepiga asisti 10.


Kwa upande wa Yanga na Azam hakuna

mchezaji hata mmoja aliyefikisha idadi ya asisti

10 ambapo kwa upande wa Yanga ni Deus

Kaseke mwenye asisti 6 na Iddy Nado mwenye

asisti 9 ambao bado wamechemsha kuwafikia

Chama na Luis.


Kwa upande wa makipa, bado Aishi Manula

amefanya vizuri kulinganisha na makipa

wengine alioshiriki ligi kuu msimu huu mara

baada ya kufanikiwa kupata 'clean sheets' 18 huku Metacha Mnata wa Yanga akiwa na clean sheets 13, jambo ambalo linawafanya Simba kuzidi kutamba.


Ukuta wa Simba pia ndio uliofungwa mabao

machache zaidi kuliko timu nyingine, ambayo ni

14 tu, wakati wanaofuata, Yanga umefungwa mabao 21 na Azam ni mabao 22.





Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: SIMBA YAIPOTEZA YANGA, AZAM FC KWENYE REKODI
SIMBA YAIPOTEZA YANGA, AZAM FC KWENYE REKODI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiffEpd7qWbG0ww8aY7AGTMdXIrStW_7r1LR-x9o2GAEu6SOsqAB3ABs8ZDnBNyePkVAUFGyVaJDy68NzG2gtQ8dgA3940ZWVBqnQuu-W4u2ZgOe95oMnFypKI6vlPk3IbLTPbscE2V_OG1/w640-h426/simbasctanzania-209227224_896182610963255_9028168401596693964_n.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiffEpd7qWbG0ww8aY7AGTMdXIrStW_7r1LR-x9o2GAEu6SOsqAB3ABs8ZDnBNyePkVAUFGyVaJDy68NzG2gtQ8dgA3940ZWVBqnQuu-W4u2ZgOe95oMnFypKI6vlPk3IbLTPbscE2V_OG1/s72-w640-c-h426/simbasctanzania-209227224_896182610963255_9028168401596693964_n.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/simba-yaipoteza-yanga-azam-fc-kwenye.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/simba-yaipoteza-yanga-azam-fc-kwenye.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy