REA yatumia zaidi ya Bil. 100 kutekeleza miradi ya umeme vijijini Kigoma
HomeHabariTop Stories

REA yatumia zaidi ya Bil. 100 kutekeleza miradi ya umeme vijijini Kigoma

Katika kuendelea kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza m...

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo June 24, 2024
Tottenham Hotspur inawania mchezaji wa kimataifa wa Brazil.
Msichomeke vitu vingi kwenye kebo moja

Katika kuendelea kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mkoa wa Kigoma.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 18 Mkoani Kigoma wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali (mstaafu), Jacob Kingu wakati wa ziara ya Bodi hiyo kukagua utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kupeleka umeme vijijini.

Wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti Kingu amewataka wakandarasi kuhakikisha wanamaliza miradi hiyo kwa wakati uliopangwa, na kwamba hawatasita kuwachukulia hatua za kimkataba mkandarasi yoyote atakayeshindwa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati kama ilivyopangwa.

“Tumeshatoa maelekezo. Hakuna muda wa nyongeza utakaotolewa kwa mkandarasi atakayeshindwa kutekeleza mradi wake ndani ya muda uliopangwa, labda kwa sababu maalum.

Tumewaelekeza wakandarasi pia wahakikishe material yote yanayohitajika kama nguzo kabla ya msimu wa mvua kuanza ili miradi hiyo isichelewe kama ilivyo dhamira ya serikali umeme kuwafikia wananchi wote ndani ya muda,” amesisitiza Mwenyekiti Kingu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Radhia Msuya amesema kuwa ziara hiyo ni muendelezo wa ziara za Bodi hiyo kuhakikisha inatembelea miradi inayosimamiwa na REA kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kubadilisha hali za wananchi wa vijijini kama ilivyo adhma ya serikali.

Akizungumza awali, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy amesema kuwa katika mkoa wa Kigoma, jumla ya Vijiji 279 kati ya Vijiji 306 katika Mkoa wa Kigoma tayari vimeunganishwa na nishati ya umeme na kusisitiza kuwa safari ya kupeleka umeme katika Vitongoji imeanza.

“Zaidi ya vitongoji 595 wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme. Katika vitongoji 1849 katika Mkoa wa Kigoma, vitongoji Zaidi ya 1370 tayari vimeshapata umeme. Tunaendelea kuhamasisha wananchi kuendelea kutumia miradi hii kutekeleza na kubuni shughuli za kiuchumi zitakazoweza kuboresha uchumi wao pamoja na kulinda miradi hii maana serikali imewekeza fedha nyingi sana,” amesema Mhandisi Saidy.

The post REA yatumia zaidi ya Bil. 100 kutekeleza miradi ya umeme vijijini Kigoma first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/mbslKjf
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: REA yatumia zaidi ya Bil. 100 kutekeleza miradi ya umeme vijijini Kigoma
REA yatumia zaidi ya Bil. 100 kutekeleza miradi ya umeme vijijini Kigoma
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/09/5e87a446-9b02-4119-8ffb-f25cf498ddf6-950x633.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/09/rea-yatumia-zaidi-ya-bil-100-kutekeleza.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/09/rea-yatumia-zaidi-ya-bil-100-kutekeleza.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy