Rais Samia Awataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Kutatua Kero za Wananchi...."Nikikuta mabango kiongozi umekwenda"
HomeHabari

Rais Samia Awataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Kutatua Kero za Wananchi...."Nikikuta mabango kiongozi umekwenda"

 Rais  wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema viongozi wa kitaifa wakikutana na mabango katika ziara zao, atawaondoa kazini mkurugenzi ...

Breaking: Rais Samia Achaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa
LIVE: Mkutano Mkuu Maalum Wa CCM, Dodoma
Taarifa Ya Kuongeza Kasi Ya Utekelezaji Wa Hatua Za Kujikinga Na Magonjwa Mbalimbali Nchini.


 Rais  wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema viongozi wa kitaifa wakikutana na mabango katika ziara zao, atawaondoa kazini mkurugenzi wa halmashauri na wakuu wa wilaya husika.

Aidha, Rais Samia amewaagiza Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na Wakuu wa Taasisi mbalimbali aliowaapisha hii leo kufanya kazi kwa kutenda haki na sio kuwanyanyasa wanaowaongoza.

Rais Samia ametoa maagizo hayo Ikulu jijini Dar es salaam alipokuwa akiwaapisha viongozi hao na kuongeza kuwa katika uongozi wake hatapenda kuona viongozi anaowateua wanawanyanyasa wanaowaongoza na jambo hilo likitokea ataamua vinginevyo.


Kuhusu kero mbalimbali za Wananchi, Rais Samia Suluhu Hassan ametaka kushughulikiwa kwa kero hizo kwa uharaka na si kusubiri viongozi wakuu akiwemo yeye mwenyewe, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.

Amesema katika ziara zake akiona bango la malalamiko ya Wananchi na utatuzi wa jambo hilo liko ndani ya uwezo wa viongozi wa ngazi ya chini, Mkuu wa wilaya ama Mkurugenzi wa  halmashauri ataondolewa katika wadhifa wake.

 “Tumezoea tunapokwenda kwenye ziara mikoani  na wilayani tunapokelewa na mabango ya wananchi wakilalamika kero mbalimbali, mabango yale mengine wala siyo mambo au masuala ya kushughulikwa katika ngazi za juu ni masuala ya kushughulikwa huko chini.

“Kwa hiyo naomba tunapokuja huko mimi na makamu wa rais, waziri mkuu tukikuta bango basi ziwe inshu ya kitaifa lakini siyo mambo ya kushughulikiwa kule chini, nataka niseme  bango moja aidha mkurugenzi au mkuu wa wilaya amekwenda na hii  haina maana mkazuie watu kuandika kero zao,” amesema.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia Awataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Kutatua Kero za Wananchi...."Nikikuta mabango kiongozi umekwenda"
Rais Samia Awataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Kutatua Kero za Wananchi...."Nikikuta mabango kiongozi umekwenda"
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiTwzLbKijbk5X8WTfgyQtacLFr-sc_aL4py5iC1kYdaSRnVwLUHipGWHdC8I87hL2A_qMNkwvAKIpi0CGUzrBFMJujSToplnlX_XBgRlQFU_ksCw8Rkv0KPZKeLTEXsnxG28zvjhYjrT9j/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiTwzLbKijbk5X8WTfgyQtacLFr-sc_aL4py5iC1kYdaSRnVwLUHipGWHdC8I87hL2A_qMNkwvAKIpi0CGUzrBFMJujSToplnlX_XBgRlQFU_ksCw8Rkv0KPZKeLTEXsnxG28zvjhYjrT9j/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/rais-samia-awataka-wakuu-wa-wilaya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/04/rais-samia-awataka-wakuu-wa-wilaya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy