HomeHabariTop Stories

MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika

Wakati Serikali ikiwa imefunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika kuanzia Mei 15 hadi Agosti 15 mwaka huu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu y...

Rais Samia aguswa na kifo cha Mwenyekiti wa CCM Liwale
Akamatwa na polisi baada ya kuvaa sare za jeshi ili akubaliwe na mpenzi wake
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 8, 2024

Wakati Serikali ikiwa imefunga shughuli za uvuvi katika Ziwa Tanganyika kuanzia Mei 15 hadi Agosti 15 mwaka huu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa, Sultan Saleh Seif, ameruhusu wananchi kuendea la shughuli hizo.

Seif alitoa kauli hiyo jana (June 26, 2024) wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ninde, Kata ya Ninde wilayani Nkasi mkoani humo.

Itakumbukwa kuwa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, akitangaza lengo la Serikali la kufunga kwa muda shughuli za uvuvi alisema lengo ni kupumzisha shughuli za uvuvi katika ziwa Tanganyika kwa miezi mitatu ili kuwezesha samaki kuzaliana na kuongeza tija kwa wavuvi wanaofanya shughuli zao ziwani humo.

Kauli za Seif zilizonukuliwa katika video fupi inayozunguka mitandaoni, ikimnukuu MNEC huyo akihamasisha wananchi kuendea na shughuli za uvuvi, inatofautiana na sababu zilizotolewa na Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdala Ulega ambaye alisema uamuzi wa Tanzania unatokana makubaliano yaliyoazimiwa katika kikao kilichofanyika mwaka 2022 kikihusisha nchi zinazozunguka ziwa hilo ambazo ni Zambia, Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Ulega alisema uamuzi huo ni utekelezaji wa Mkataba wa Kikanda wa Nchi Wanachama wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika unaoweka hatua na taratibu za usimamizi endelevu wa shughuli za uvuvi katika ziwa hilo.

Aliongeza uamuzi huo unatokana na utafiti uliobainisha kuwa kumekuwepo na upungufu mkubwa wa samaki na dagaa katika ziwa Tanganyika kunakotokana na ongezeko kubwa la uvuvi usio endelevu uliopelekea uharibifu wa mazalia ya samaki.

The post MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/etiKDvw
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika
MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/06/mnec-ccm-rukwa-atofautiana-na-serikali.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/06/mnec-ccm-rukwa-atofautiana-na-serikali.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy