HomeHabariTop Stories

Akamatwa na polisi baada ya kuvaa sare za jeshi ili akubaliwe na mpenzi wake

Mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemuhukumu kifungo cha miezi sita Rajabu Reli (22), mkazi wa Sengerema baada ya kukutwa na ha...

Watu wasiopungua 20 wafariki kwenye ajali ya ndege Sudan Kusini
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 30, 2024
Jiji la Arusha lafanya tukio kubwa,mitambo ya billion 1.7 yanunuliwa kukarabati barabara zote

Mahakama ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza imemuhukumu kifungo cha miezi sita Rajabu Reli (22), mkazi wa Sengerema baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)

Hukumu hiyo imetolewa January 7, 2025 katika shauri la jinai namba 445 la mwaka 2025 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Evodius Kisoka mbele ya mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa na mwendesha mashtaka wa Serikali Nyamhanga Tissoro mbele ya hakimu Evodius Kisoka, mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 05.12.2024 kijiji cha Kasisa, wilaya ya Sengerema kinyume na kifungu cha 178(1) cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani januari 07.2025 na kusomewa shitaka la kuvaa sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania bila ruhusa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kusikiliza pande zote za ushahidi hakimu Evodius Kisoka alijiridhisha kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ni mzito na haukuacha shaka lolote.

Hata hivyo, mshtakiwa alipopewa nafasi ya kujitetetea kwanini asipewe adhabu; aliomba mahakama hiyo imuachie huru kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na alivaa ili akubaliwe na mchumba wake.

Ombi hilo lilitupiliwa mbali na Hakimu Kisoka na kutoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama ya Rajabu.

 

The post Akamatwa na polisi baada ya kuvaa sare za jeshi ili akubaliwe na mpenzi wake first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/jEHdglJ
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Akamatwa na polisi baada ya kuvaa sare za jeshi ili akubaliwe na mpenzi wake
Akamatwa na polisi baada ya kuvaa sare za jeshi ili akubaliwe na mpenzi wake
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/akamatwa-na-polisi-baada-ya-kuvaa-sare.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/akamatwa-na-polisi-baada-ya-kuvaa-sare.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy