Rais Samia aguswa na kifo cha Mwenyekiti wa CCM Liwale
HomeHabariTop Stories

Rais Samia aguswa na kifo cha Mwenyekiti wa CCM Liwale

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na Kif...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo September 19, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo September 19, 2024
Kapinga afungua kikao kazi TPDC

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na Kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Liwale Ndugu. Kindamba Milingo.

Akiwasilisha salamu za Chama cha Mapinduzi kwa waombolezaji waliojitokeza katika Msiba huo Uliofanyika leo (Jumatano, Januari 08, 2025) Nyumbani kwa Marehemu Pulipwite Liwale Mjini mkoani Lindi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais anatambua mchango mkubwa uliofanywa na marehemu enzi ya uhai wake katika kukijenga Chama cha Mapinduzi.

“Kwa niaba ya Mwenyekiti wetu wa Chama, Katibu Mkuu na viongozi wengine naomba kuwasilisha salamu za rambirambi kutoka Chama cha Mapinduzi CCM, viongozi wetu hawa wote wameguswa na kifo cha Milingo na wanatambua kazi kubwa aliyoifanya katika kukijenga chama kwenye ngazi ya Wilaya alipokuwa anahudumu”

Amesema marehemu mzee Milingo alikuwa kiunganishi kikubwa kati ya Chama na Serikali katika kuhakikisha wanafuatilia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili kusaidia kuongeza kasi ya maendeleo ndani ya Wilaya ya Liwale.

Mheshimiwa Majaliwa amesema ni vyema wanachama wa CCM wakaendelea kuenzi mazuri yote yaliyofanywa na Mwenyekiti huyo pamoja na kuendelea kumuombea.

“Mzee wetu amefanya kazi kubwa ndani ya chama, yeye pamoja na viongozi wengine walikiunganisha Chama na Mkoa wa Lindi.

Naye Mbunge wa Liwale Zuberi Kuchauka amesema Wilaya ya Liwale imepoteza kiongozi Mahiri na Mwanachama Mtiifu wa Chama cha Mapinduzi ambaye alijitoa kwa nguvu zote kukijenga chama hicho.

Marehemu Mzee Milingo alifariki tarehe 6 Januari 2025 katika hospitali ya Rufaa ya Sokoine Mkoani Lindi, amezikwa katika makaburi ya Nanganda Liwale Mkoani Lindi.

The post Rais Samia aguswa na kifo cha Mwenyekiti wa CCM Liwale first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/Kb7lUEB
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia aguswa na kifo cha Mwenyekiti wa CCM Liwale
Rais Samia aguswa na kifo cha Mwenyekiti wa CCM Liwale
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250108-WA0020-950x552.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/rais-samia-aguswa-na-kifo-cha.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/rais-samia-aguswa-na-kifo-cha.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy