PATRICK Aussems maarufu kwa jina la uchebe ambaye aliweza kuifundisha timu ya Simba kwa mafanikio makubwa anatajwa kuingia kwenye rada za...
PATRICK Aussems maarufu kwa jina la uchebe ambaye aliweza kuifundisha timu ya Simba kwa mafanikio makubwa anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga.
Kwa sasa kikosi cha Yanga ambacho kinaongoza Ligi Kuu Bara kikiwa na pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23 kipo chini ya Juma Mwambusi.
Cedric Kaze aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo baada ya kuongoza kwenye mechi 18 za ligi akishinda 10, sare 7 na kupoteza moja amechimbishwa kikosii hapo Machi 7 kutokana na kile ambacho kimeelezwa kuwa mwendo mbovu wa timu hiyo.
Aussems kwa sasa yupo nchini Kenya anakinoa kikosi cha AFC Leopards hivyo ikiwa Yanga watakuwa kwenye hesabu za kumpata itawalazimu kuvunja mkataba wake ndani ya kikosi hicho.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa kwa sasa wameanza mchakato wa kumtafuta mrithi wa Kaze na wanaamini kwamba watampata hivi karibuni.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS