Changamoto Za Wafanyakazi Trc Na Tazara Kupatiwa Ufumbuzi
HomeHabari

Changamoto Za Wafanyakazi Trc Na Tazara Kupatiwa Ufumbuzi

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Atupele Mwakibete, amesema Sekta ya Uchukuzi iko katika hatua mbalimbali za kushughulikia ...

“Serikali Ya Rais Samia Imejipanga Kuimarisha Sekta Ya Viwanda Na Biashara “ -Dkt.Hashil Abdalah
Naibu Waziri Mabula: Zingatieni Masharti Ya Umiliki Ardhi
Wajasiliamali Wahimizwa Kutengeneza Bidhaa zenye Ubora


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Atupele Mwakibete, amesema Sekta ya Uchukuzi iko katika hatua mbalimbali za kushughulikia changamoto  za watumishi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Mamlaka ya Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kuongeza tija kwa taasisi hizo.

Naibu Waziri Mwakibete ametoa kauli hiyo alipotembelea  karakana ya kutengeneza vichwa na mabehewa ya TRC Mkoani Morogoro na kusisitiza Serikali itaendelea kuwekeza kwenye taasisi hizo ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji nchini.

“Changamoto za kitumishi ambazo zimekuwa zikiendelea hapa nataka niwahakikishie kuwa zitatatuliwa na mtapata mrejesho kupitia viongozi wa taasisi, ninaamini zikishughulikiwa kwa kiasi kikubwa zitachangia mabadiliko kiutendaji” amesema Naibu Waziri Mwakibete.

Naibu waziri Mwakibete ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wafanyakazi wa karakana hiyo kwa kufanya kazi kwa weledi na kujituma wakiwa na lengo la kuhakikisha kazi hazisimami katika karakana hiyo.

Aidha, Naibu Waziri Mwakibete amewasisitiza watumishi hao kufanya ukarabati wa vichwa na mabehewa kwa kuzingatia thamani ya fedha ili uwekezaji unaofanywa ufanyike kwa makini ili kufanya viendelee kutoa huduma za uhakika na salama.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Albert Magandi, amesema mpaka sasa kupitia watumishi hao wameweza  kukarabati vichwa vya treni takribani kumi na Sita  kwa ajili  kusafirisha mizigo na abiria na vichwa saba kwa ajili ya treni za sogeza.

Naye Mmoja wa watumishi  wa karakana hiyo, Bw. Vedastus Lugega, amemweleza Naibu Waziri huyo kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo Wafanyakazi  wako tayari kuendelea kuhakikisha ukarabati unafanywa kwa wakati na kuzingatia viwango ili kutohujumu Serikali.

Naibu Waziri Mwakibete yuko Mkoani Morogoro kwa ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya miradi ya sekta ya uchukuzi ikiwemo mradi wa ukarabati wa vichwa na mabehewa.

(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi)



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Changamoto Za Wafanyakazi Trc Na Tazara Kupatiwa Ufumbuzi
Changamoto Za Wafanyakazi Trc Na Tazara Kupatiwa Ufumbuzi
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgKmzmEbCMih8dm1hBQYqXDXeR357Y9bihuD3k1aj5hPQygIHuSgRGhYItkZJYVHhYI0_goSPB9aqFH4ej2ugOHJ_WvYyz37tvsdp-8HXaGS3QZj4fzk0fBVIx9NykcJmWZ98T9jBaO4tk6tesAIo8RKu51Xw2DRNFX-Be2hkAX7bdQTEDKFzEUc9iwbw=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgKmzmEbCMih8dm1hBQYqXDXeR357Y9bihuD3k1aj5hPQygIHuSgRGhYItkZJYVHhYI0_goSPB9aqFH4ej2ugOHJ_WvYyz37tvsdp-8HXaGS3QZj4fzk0fBVIx9NykcJmWZ98T9jBaO4tk6tesAIo8RKu51Xw2DRNFX-Be2hkAX7bdQTEDKFzEUc9iwbw=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/changamoto-za-wafanyakazi-trc-na-tazara.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/changamoto-za-wafanyakazi-trc-na-tazara.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy