Serengeti Music Festival Sasa Siku Mbili- Dkt. Abbas
HomeHabari

Serengeti Music Festival Sasa Siku Mbili- Dkt. Abbas

Na. John Mapepele Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hassan Abbas amesema Tamasha kubwa la kihistoria la Muziki lijulikanalo ka...


Na. John Mapepele

Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hassan Abbas amesema Tamasha kubwa la kihistoria la Muziki lijulikanalo kama Serengeti Music Festival la mwaka huu limeongeza siku ambapo sasa litafanyika kwa siku mbili badala ya moja kama ilivyopangwa awali kutokana na mahitaji makubwa ya tamasha hilo kwa wasanii na wananchi.

Akizungumza na Kamati ya Maandalizi yaTamasha hilo  Machi 1, 2022 jijini Dar es Salaam amesema kuongezeka kwa siku hizo kunatokana na wasanii wengi kuomba kushiriki katika tamasha la mwaka huu ambalo litafanyika kuanzia Machi 12-13, 2022 jijini Dodoma.

“Mwitikio wa wasanii tulioupata katika msimu huu ni mkubwa sana ambapo hadi sasa wasanii wakongwe na chipukizi zaidi ya mia moja wameomba kushiriki tamasha hili kutokana na jinsi ambavyo limekuwa likiandaliwa vizuri na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali” . Amefafanua Dkt. Abbas

Aidha, Dkt. Abbasi amesema kuwa Tamasha hili ndiyo tamasha pekee kubwa linalowaleta pamoja wasanii mbalimbali, wachanga na wakongwe, pia bendi za muziki kujumuika pamoja bila kujali lebo zao.

Ameongeza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha wasanii wanabadilishana uzoefu kwenye fani ya muziki ili kukuza vipaji vyao huku wakitumia tamasha hilo kutangaza utalii na vivutio mbalimbali vya Tanzania.

“Tamasha hili tumelipa jina la Serengeti kwa dhumuni la kuonyesha na kurithisha sanaa ya muziki kwa vizazi vya sasa na baadaye lakini pia kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii kupitia Mbuga ya Serengeti .” Ameongeza Dk. Abbas

Pia amesema tofauti na matamasha mengine wasanii wote wanaoshiriki tamasha hili wanapata fursa ya kufundishwa na wataalam mambo mbalimbali kabla ya kufanya maonesho yao.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serengeti Music Festival Sasa Siku Mbili- Dkt. Abbas
Serengeti Music Festival Sasa Siku Mbili- Dkt. Abbas
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEi6HaTm-lf0tnSGM7-PDcW1yeyuB1NZe25nAMMEbhl9ttpatBLPKarIVVbj4CbGd5n8jrVuhnv8VXB2_jbVvH2UAnTOBqmFKYUQjjsZW4dDMFtx5c-WMMP7njMK9hczTBAH_HYarqw7Goti4BpYct_EA-Y28hq_lJKKpX-iJbkK0Y0EehEYPLK_6WgweA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEi6HaTm-lf0tnSGM7-PDcW1yeyuB1NZe25nAMMEbhl9ttpatBLPKarIVVbj4CbGd5n8jrVuhnv8VXB2_jbVvH2UAnTOBqmFKYUQjjsZW4dDMFtx5c-WMMP7njMK9hczTBAH_HYarqw7Goti4BpYct_EA-Y28hq_lJKKpX-iJbkK0Y0EehEYPLK_6WgweA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/serengeti-music-festival-sasa-siku.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/serengeti-music-festival-sasa-siku.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy