KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Yahya Zayd, anatarajia kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita baada ya kupata majeraha ya bega kweny...
KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Yahya Zayd, anatarajia kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita baada ya kupata majeraha ya bega kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City.
Zayd kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex alitengeneza pasi ya bao la pili lililofungwa na Prince Dube.
Hakuweza kumaliza dakika zote 90 kwa kuwa alilazimika kutolewa kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza, baada ya kupata majeraha hayo baada ya kufanyiwa madhambi wakati akielekea kufunga.
Mchezo huo ulikamilika kwa Azam FC 2-1 Mbeya City na kusepa na pointi tatu jumlajumla.
Kwa msimu wa 2020/21, Azam FC imekusanya pointi zote sita mbele ya Mbeya City na kuifunga jumla ya mabao matatu, mchezo wa kwanza ilishinda bao 1-0 Uwanja wa Sokoine Mbeya na wa pili ilishinda mabao 2-1.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 20 ina pointi 36.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS