Wakurugenzi Na Wakuu Wa Wilaya Kupimwa Kwa Utendaji Kazi Wao
HomeHabari

Wakurugenzi Na Wakuu Wa Wilaya Kupimwa Kwa Utendaji Kazi Wao

Na Angela Msimbira OR – TAMISEMI Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Innocent Bashungwa amesema kuwa W...


Na Angela Msimbira OR – TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Innocent Bashungwa amesema kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Wilaya watapimwa kutokana na utendaji kazi wao wa kuhakikisha wanatatua kero za wananchi.

Akiongea na viongozi wa Mkoa wa Njombe  Waziri Bashungwa amesema moja ya kigezo cha kuwapima Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya ni kasi ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri, amewaagiza kuhakikisha wanaongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato

Ameongeza kuwa fedha nyingi zinatolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo hivyo ni wajibu wa viongozi hao kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha hizo, hivyo nitoe wito kwa Wakurugenzi Wakuu wa Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha hizo kwa uaminifu.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuamini vijana katika kumesaidia kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi hivyo Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya tusimuangushe na Mimi nikiwa ni Waziri mwenye dhamana sitakubali kumuangusha” amesisitiza Waziri Bashungwa

Waziri Bashungwa amesisitiza Wakurugenzi kuhakikisha wanajibu hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa asilimi 100 na kuhakikisha fedha zinazokusanywa zinawekwa benki kwa wakati na kuacha tabia ya kutumia fedha mbichi,

Ameongeza kuwa kigezo kingine ni utoaji wa Mikopo ya asilimia kumi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu amewataka kuhakikisha fedha inayotolewa inaenda kwenye miradi yenye tija ya kuwasaidia waliopewa, amewataa Viongozi hao kutoa ushauri wa namna bora ya kukusanya fedha zilizotolewa.

Aidha amewaagiza wakuu wa Mikoa wote nchini kuhakikisha wanasimamia utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuhakikisha fedha hizo zinaenda kwenye miradi yenye tija na kama kuna ujanja unaofanywa na Halmashauri au idara inayoshughulikana mikopo wafuatilie na kutoa taarifa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuwa hicho piano kigezo kingine cha kuwapima Wakurugenzi katika Halmashauri kwa kuangalia wanasimamia vipi utoaji wa mikopo ya asilimia kumi



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Wakurugenzi Na Wakuu Wa Wilaya Kupimwa Kwa Utendaji Kazi Wao
Wakurugenzi Na Wakuu Wa Wilaya Kupimwa Kwa Utendaji Kazi Wao
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjH88xDlYm0MOyQC1_Djx3to3YG-FRL8i-kPkd1BaalM-XGOHVVVDqRH4CcuPulgpAxMmCflQBZDm2kSE3HQp1b8FHw-yKYAHZJ9O0WPvz_h22Dl6brvqjObiFMlFO_OxXoP6VeVZWnbWFeEO8c63IimWGBChdtSNCYeGLymyqQ9YyBePs49H5JK8J4VA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjH88xDlYm0MOyQC1_Djx3to3YG-FRL8i-kPkd1BaalM-XGOHVVVDqRH4CcuPulgpAxMmCflQBZDm2kSE3HQp1b8FHw-yKYAHZJ9O0WPvz_h22Dl6brvqjObiFMlFO_OxXoP6VeVZWnbWFeEO8c63IimWGBChdtSNCYeGLymyqQ9YyBePs49H5JK8J4VA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/wakurugenzi-na-wakuu-wa-wilaya-kupimwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/wakurugenzi-na-wakuu-wa-wilaya-kupimwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy