Wachezaji wa Simba wakimpongeza Hajibu kwa kufunga bao Simba SC leo hii imetoa kichapo cha bao 2-1 kwa Kagera sugar ...
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Hajibu kwa kufunga bao
Katika kipindi cha kwanza timu hizo zilitoka suluhu bin suluhu.
Katika Kipindi cha pili, Simba SC walianza mpira kwa kasi na kwenye dakika ya 52 mshambuliaji Ramadhani Singano alipeleka kilio kwa Kagera baada ya kufunga bao zuri lakini kwenye dakika ya 63 Kagera sugar walisawazisha bao kupitia kwa mchezaji Rashid Mandawa, hata hivyo bao hilo alikudumu kwenye dakika ya 71 Ibrahim Hajib aliwainua tena mashabiki wa Simba baada ya kufunga bao kwa mkwaju wa penati kufuati mlinzi wa Kagera Sugar kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Mshambuliaji wa Kagera sugar Rashindi ameshika nafasi ya pili kwa wafungaji bora wa mabao katika ligi kuu bara baada ya leo kufikisha mabao 10 sambamba na Didier Kavumbagu wa Azam FC huku wote wakiwa nyuma ya mshambuliaji wa Yanga Simon Msuva ambaye ana mabao 11 mpaka sasa.
COMMENTS