Najua watu wengi waliisubiri hii kwa hamu.. wengine hata sio mashabiki wa boxing lakini walijikuta wakivutiwa na hii.. Promo ilikuwa kubw...
Najua watu wengi waliisubiri hii kwa hamu.. wengine hata sio mashabiki wa boxing lakini walijikuta wakivutiwa na hii.. Promo ilikuwa kubwa sana, pambano la kihistoria ambalo dunia nzima ililisubri ni hili kati ya Floyd ‘Money’ Mayweather na Manny Pacquiao.
Points tayari zimeamua, pambano limeenda kwa round 12, Floyd Mayweatherkamshinda Pacquiao kwa points sita tu.. Floyd ana points 117 na Pacquiao ana points 111.
Kwa matokeo hayo Mayweather kaendeleza kuweka rekodi yake kubwa ya kutoshindwa pambano hata moja tangu amekuwa professional boxer.
Mayweather akimtwanda konde Manny Pacquiao (kulia) katika pambano lilofanyika bustani ya MGM Las vegas, Marekani.
HATIMAYE mzizi wa fitina
umekatwa baina ya Floyd Mayweather dhidi ya Manny Pacquiao asubuhi hii
na bingwa asiyepigika Mayweather ameibuka kidedea kwa pointi.
Pacquiao (kulia) alikuwa kinara
wa kurusha makonde, lakini Mayweather alicheza kijanja na kurusha
makonde ya uhakika na kuwashawishi majaji.
Mayweather ameshinda kwa pointi 118-110, 116-112, 116-112
Ni pambano ambalo mashabiki masumbwi walifikiri hawaji kuliona na limekuwa likishindikana kwa miaka mitano iliyopita, lakini limechezwa mwaka huu 2015.
Sasa Mayweather ameendeleza rekodi ya kutopigwa katika mapambano 48 na leo hii amecheza kwa kiwango kizuri dhidi ya Mbunge Pacquiao.
Pambano hilo kubwa la Karne limepigwa La Vegas Marekana na lilikuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 300.
COMMENTS