ASKARI WANNE WAJERUHIWA KWA RISASI MKOANI TANGA
HomeHabariKitaifa

ASKARI WANNE WAJERUHIWA KWA RISASI MKOANI TANGA

Askari wanne wa jeshi la polisi Tanzania wamejeruhiwa kwa risasi baada ya kutokea mapigano kati yao na watu wa...


Askari wanne wa jeshi la polisi Tanzania wamejeruhiwa kwa risasi baada ya kutokea mapigano kati yao na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika mapango ya Amboni mkoani Tanga nchini Tanzania.
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi la Polisi CP Paul Chagonja
Akitoa taarifa rasmi ya jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi la Polisi CP Paul Chagonja aliyelazimika kusafiri kwa helkpta kutoka Dar es salaam kwenda Tanga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa si tukio kubwa kama linavyoelezwa na baadhi ya watu na kwamba waliohusika ni majambazi na siyo magaidi.

Amesema kilichotokea ni oparesheni ya kawaida iliyofanywa na jeshi la polisi kuwasaka watu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliodaiwa kujificha katika mapango hayo na ndipo yalipotokea mapigano hayo yaliyoambatana na kurushiana risasi na kupelekea askari hao kujeruhiwa.
Amesema baada ya hali kuwa tete, jeshi hilo lililazimu kuomba msaada kutoka kwa askari wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ ambao walifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kutuliza hali ya taharuki iliyokuwa imetanda katika eneo hilo.
Kamishna Chagonja amesema askari waliojeruhiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo, na kwamba jeshi hilo linaendelea na msako ambapo hadi sasa hakuna alikamatwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda ambao ni watu wanaoishi maeneo ya jirani na mapigano hayo pamoja na mwanahabari wetu, wamesema kuwa mapigano hayo yaliyoanza jana usiku na kuendelea hadi usiku kucha na kwamba mwanajeshi mmoja wa JWTZ anahofiwa kuuawa na mwili wake umepelekwa katika hospitali hiyo ya Bombo.
Alipoulizwa kuhusiana na madai ya kuwepo kwa kifo cha mwanajeshi mmoja, CP Paul Chagonja amesema kuwa Jeshi la Polisi halina mamlaka ya kutoa taarifa inayohusu wanajeshi wa JWTZ, na kuwataka wanahabari waulizie suala hilo kwa msemaji wa JWTZ.
Tumemtafuta msemaji wa JWTZ Meja Joseph Masanja ambaye amesema kuwa si jukumu lake kutoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo, kwa kuwa tukio hilo ni la kipolisi na siyo la kijeshi.
“Ukitaka kujua taarifa yoyote kuhusu tukio hilo waulize polisi, kwa kuwa hilo ni tukio la kipolisi, sisi huku hatuna taarifa yoyote” amesema Meja Masanja.
Mwanahabari wetu alipotaka kupata taarifa zaidi kutoka katika hospitali ya Bombo ameambiwa kuwa polisi imewazuia kutoa taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo.
Alipojaribu kumuuliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Said Magalula kuhusu kifo cha mwanajeshi mmoja, Mkuu huyo wa mkoa alikiri kupata taarifa za kifo hicho bila kueleza zaidi.
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: ASKARI WANNE WAJERUHIWA KWA RISASI MKOANI TANGA
ASKARI WANNE WAJERUHIWA KWA RISASI MKOANI TANGA
http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=226825&d=1423909211
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/02/askari-wanne-wajeruhiwa-kwa-risasi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/02/askari-wanne-wajeruhiwa-kwa-risasi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy