Kocha Mkuu wa Azam FC, Joseph Omog AZAM leo inatarajiwa kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa itakapome...
Mechi hiyo ni ya kisasi baada ya El Merreikh kuifunga Azam kwa mikwaju ya penalti 4-3 katika mechi ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Kagame iliyofanyika Kigali, Rwanda Agosti mwaka jana baada ya kutoka sare katika muda wa kawaida wa dakika 90.
Mabingwa hao wa Tanzania Bara wanashiriki michuano ya kimataifa kwa mara ya pili, mwaka jana walishiriki Kombe la Shirikisho na kuishia raundi ya awali baada ya kutolewa na Ferroviario de Nampula ya Msumbiji.
Akizungumzia mechi hiyo, kocha wa Azam Joseph Omog alisema amekiandaa kikosi chake vizuri na hana shaka ya kuibuka na ushindi leo. Alisema anatambua ugumu wa mechi hiyo lakini amewaelekeza wachezaji wake cha kufanya na kupata matokeo mazuri.
“Najua kuwa mechi yetu kesho (leo) itakuwa ngumu sana kwa sababu kila timu itataka kushinda mechi ya kwanza lakini wachezaji wangu wanajua cha kufanya,” alisema.
Azam inaingia uwanjani leo ikitoka kupata ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mechi ya Ligi Kuu bara wiki iliyopita.
COMMENTS