Kikosi cha Yanga kilichoanza leo YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani...
YANGA SC imeendeleza wimbi la
ushindi katika michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani
Zanzibar kwenye uwanja wa Amaan baada ya kuitandika mabao.. timu ya
Polisi.
Mbrazil Andrey Coutinho alikuwa
wa kwanza kuiandikia Yanga bao la kuongoza katika dakika ya 27 ya
kipindi cha kwanza na baadaye dakika ya 33 Mliberia Kpha Sherman
aliandika kimiani bao la pili akimalizia mpira mzuri aliotengewa kwa
njia ya kichwa na Amissi Tambwe.
kikosi cha Polisi kilichoanza leo |
Katika dakika ya 56 ya kipindi cha pili, Coutinho aliandika bao la tatu kwa mpira wa adhabu ndogo.
Katika day a 80 Saimon Msuva aliandika bao la nne akimalizia pasi nzuri ya Salum Telela.
Hilo ni bao la nne la Msuva katika mechi mbili tu za mashindano ya Mapinduzi 2015.
Huo ni ushindi wa pili kwa Yanga
kwani katika mechi ya kwanza iliyopigwa juzi uwanja wa Amaan, vijana hao
wa Hans Van der Pluijm waliitandika Taifa ya Jang’ombe mabao 4-0 ambapo
Saimon Msuva alipiga mabao matatu ‘hat-trick’ na moja likifungwa na
Sherman.
Yanga chini ya Pluijm
wamebadilika kiuchezaji ambapo wanashambulia zaidi tofauti na kipindi
cha Marcio Maximo aliyekuwa anatumia mbinu za kujihami zaidi.
Mbali na kushambulia, Yanga wanacheza mpira wa kupasiana kwa dakika zote 90 na kupanga mashambulizi ya maana.
Baada ya mechi hii, majira ya saa
2:00 usiku, mabingwa watetezi wa Tanzania bara, Azam fc watachuana
vikali na KMKM ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan.
Michuano hiyo itaendelea kesho
kwa mechi mbili kupigwa uwanja wa Amaan ambapo Mafunzo wataoneshana kazi
na Mtibwa Sugar fc majira ya saa 11:00 jioni na usiku saa 2:00, Simba
watachuana na JKU.
kikosi cha Polisi kilichoanza leo

COMMENTS