Majaliwa: Jitihada Zinahitajika Kutokomeza Unyanyasaji
HomeHabari

Majaliwa: Jitihada Zinahitajika Kutokomeza Unyanyasaji

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema jitihada za pamoja zinahitajika ili kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vikiwemo vya ukek...

Kamati ya bajeti ya baraza la wawakilishi ZNZ yapongeza miradi ya ujenzi ya miundombinu ya mabasi yaendayo haraka daraja la juu
Picha: Rais Samia ahudhuria uzinduzi wa Utalii wa Kasa Kizimkazi, Visiwani Zanzibar
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 24, 2024


 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema jitihada za pamoja zinahitajika ili kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vikiwemo vya ukeketaji kwani madhara yake ni makubwa.

Pia, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum isimamie utekelezaji wa mipango na mikakati mahsusi ya kutokomeza ukeketaji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Ijumaa, Februari 18, 2022) wakati akiahirisha Mkutano wa Sita wa Bunge la 12 Bungeni Jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi tarehe 5 Aprili 2022.

Amesema vitendo vya ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto vinaendelea licha ya uwepo wa afua mbalimbali za kuelimisha wananchi kuhusu madhara yake.

Ameongeza kuwa mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukeketaji ni Manyara (asilimia 58),  Dodoma (asilimia 47), Arusha (asilimia 41), Mara (asilimia 32) na Singida (asilimia 31).

Amesema takwimu hizo zinaonesha kuwa bado suala hilo ni changamoto kwa nchi yetu, hivyo ametoa wito kwa viongozi mbalimbali kuhamasisha wananchi kupinga vitendo hivyo vya ukatili.

“Nitoe wito kwa Waheshimiwa Wabunge wenzangu, Viongozi wa Dini na wadau wote kuunganisha nguvu na kukemea vitendo hivyo, pia hatua kali zichukuliwe kwa wanaojihusisha na vitendo hivyo.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameliagiza Jeshi la Polisi nchini liongeze nguvu ya kiulinzi hadi kwenye ngazi ya kata, kufanya operesheni na misako ya kuwabaini wahalifu wote.

“Fanyeni operesheni na misako ya kuwabaini wahalifu wote wakiwemo waganga wanaopiga ramli chonganishi na kuchukulia hatua askari, wakaguzi na maafisa wasio waadilifu.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kujitokeza kwa matukio mbalimbali ya hivi karibuni yanayohusisha mauaji ya raia kwa raia, moto kwenye masoko na baadhi ya raia kujinyonga.

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa taasisi za dini waendelee kusaidia katika suala zima la malezi ya kiroho ili kujenga jamii yenye uchamungu na uadilifu.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Majaliwa: Jitihada Zinahitajika Kutokomeza Unyanyasaji
Majaliwa: Jitihada Zinahitajika Kutokomeza Unyanyasaji
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhTznju942SFeAjwaDq_T2ZbzVPHnxPOX9t_bAcW5hWR5dDrAOXvpXQq4nN4vDQlTHJnPVBs44ODsPRt-IRd8fcGeA8LUDRxD72X0XZkMBVSoSmPzEyiuZgOAmUBV-U88olV0_l6EcUt9v-MTg4ZdylKsej8AODlQKmY8nzoGE4vjsuxuS7m1AqumF-Eg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhTznju942SFeAjwaDq_T2ZbzVPHnxPOX9t_bAcW5hWR5dDrAOXvpXQq4nN4vDQlTHJnPVBs44ODsPRt-IRd8fcGeA8LUDRxD72X0XZkMBVSoSmPzEyiuZgOAmUBV-U88olV0_l6EcUt9v-MTg4ZdylKsej8AODlQKmY8nzoGE4vjsuxuS7m1AqumF-Eg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/majaliwa-jitihada-zinahitajika.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/02/majaliwa-jitihada-zinahitajika.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy