Wahusika katika sakata la Escrow wakitinga katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakiongozwa na polisi na mawakili ...
Vigogo waliofikishwa mahakamani hapo leo, kutoka Benki Kuu Tanzania (BoT) Steven Urassa, Shirika la umeme (Tanesco) Kyabukoba Rutabingwa, na kutoka Mamlaka ya Mapato ( TRA) ni Julius Angelo ambaye amekosa dhamana.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imeitupia zigo ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ili kuchukua hatua ya kuwafikisha mahakamani vigogo wote wakiwamo mawaziri.
Pamoja na wengine watakaobainika kwenye uchunguzi wake nakukutwa na hatia ya kuhusika na vitendo vya rushwa katika sakata la uchotwaji wa sh202bilioni katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Chanzo MWANANCHI
COMMENTS