Meli yaua 14, basi laua 4
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda
HomeMatukio

Meli yaua 14, basi laua 4

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda WATU 18 wamepoteza maisha katika ...

WATU 18 wamepoteza maisha katika ajali mbili tofauti, ambapo katika ajali ya majini meli iliyobeba shehena ya mahindi imezama na kuua watu 14, wakati katika ajali ya barabarani, basi kutoka Handeni mkoani Tanga kwenda Dar es Salaam limeua watu wanne.
Meli yazama Katika ajali ya majini, Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema abiria 14 kutoka nchi jirani ya Burundi wanahofiwa kufa maji baada ya meli ya mizigo waliyokuwa wakisafiria, kuzama eneo la kijiji cha Kala mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
Kamanda alisema meli hiyo ni Mv Mbaza na ilisajiliwa Burundi. Ilikuwa na shehena ya mahindi tani 437 na watu 15.

Alisema meli hiyo iliondoka katika bandari ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa Januari 10 mwaka huu kati ya saa 5 na 6 usiku na saa mbili baadaye ilizama eneo la kijiji cha Kala.
“Taarifa zilizopo ambazo zimethibitishwa na wamiliki wa meli hiyo waliopo Burundi ni kwamba wafanyakazi 13 kati ya 14 wa meli hiyo na abiria mmoja wanahofiwa kufa maji,” alieleza.
Kamanda alisema ni mfanyakazi mmoja pekee ndiye aliyeokolewa na meli nyingine ya Burundi iitwayo Mv Teza, iliyokuwa ikitokea bandari ya Mpulungu nchini Zambia ikielekea nchini Burundi.

“Mtu huyo aliokolewa Januari 13, mwaka huu ambapo hadi sasa bado hajapata fahamu...hivyo kushindwa kupata taarifa za chanzo cha ajali hiyo,” alisema. Kamanda Mwaruanda alisema hadi sasa hakuna mwili wowote ule ulioopolewa wala kuonekana.
Alisema hapakuwepo na mawasiliano ya redio kati ya bandari na meli hiyo, kwani bandari hiyo ya Kasanga haina mawasiliano yoyote, zaidi ya simu za mkononi.

“Maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika vikiwemo vijiji vya Kala, Wampembe na Mpasa wilayani Nkasi hakuna mawasiliano yoyote yale ya simu. Meli hiyo iliruhusiwa kuondoka usiku katika bandari ndogo ikiwa haina vifaa vyovyote vya mawasiliano,” alisema.
Ofisa Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) mkoa wa Rukwa, David Charagi alieleza kuwa meli hiyo ilifuata taratibu zote za ukaguzi katika forodha ya Kasanga na kuruhusiwa kuendelea na safari.

Basi la Hajees John Gagarini anaripoti kutoka Kibaha kuwa, watu wanne wamekufa baada ya basi kampuni ya Hajees, walilokuwa wakisafiria kutoka Handeni kwenda Tanga kuacha njia na kupinduka.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 2:00 katika kijiji cha Mnazi, kata ya Mandela wilayani Bagamoyo na ilihusisha basi hilo, aina ya Scania lenye namba za usajili T 834 BAU.

Alisema basi hilo lilipinduka na watu hao wanne walikufa papo hapo.
Alitaja waliokufa ni kondakta wa basi hilo, Mkomwa Juma (35) mkazi wa Kimange, Siasa Iddi (25) mkazi wa Kwamakocho, Mayunga Ramadhan (45) na Rehema Omar 35. Miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Meli yaua 14, basi laua 4
Meli yaua 14, basi laua 4
http://www.habarileo.co.tz/images/resized/images/kamanda-jacob-mwaruanda_300_173.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/meli-yaua-14-basi-laua-4.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/meli-yaua-14-basi-laua-4.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy