UWT wamshika mkono kijana mwenye ulemavu wilayani Makete
HomeHabariTop Stories

UWT wamshika mkono kijana mwenye ulemavu wilayani Makete

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Dkt.Skolastika Kevela ameitaka jamii kuendelea kusaidia watu wenye uhitaji kupunguza changamoto wanazokumba...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo August 30, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 30, 2024
Picha:Rais Samia akizindua ndege za mafunzo ya awali ya marubani na mabasi kwa JWTZ

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Dkt.Skolastika Kevela ameitaka jamii kuendelea kusaidia watu wenye uhitaji kupunguza changamoto wanazokumbana nazo hali inayoweza kuwarejeshea tabasamu na kujiona watu wa muhimu katika jamii.

Dkt.Skolastika Kevela ametoa kauli hiyo wakati akitoa msaada kwa familia ya Nicko Mbwilo mkazi wa mamlaka ya mji mdogo wa Iwawa ambaye mtoto wake wa umri wa miaka 21 Amos Mbwilo amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa TB na Uti wa mgongo kwa muda mrefu sasa.

“Mtoto kama huyu tukimpa thawabu yetu inaandikwa mbinguni na tukumbuke mwenyezi Mungu akikupa basi kata kidogo na upeleke kwa wahitaji”amesema Dkt.Kevela

Rehema Pella ambaye ni mama wa mtoto na Niko Mbwillo baba wa familia wamesema mtoto huyo hajiwezi kwa huduma za msingi hivyo kulazimika kumhudumia Kwa Kila kitu ikiwemo kumpeleka maliwatoni.

“Pia amepata vidonda mpaka mgongoni sasa uwezo wa kukaa na kulala sana hana tunabaki tunamgeuza usiku na mchana ninapoenda kwenye kazi za mikono mwenzangu anabaki na kijana lakini pia alizaliwa na jicho dogo ila TB ndio iliyomsumbua”amesema Rehema Pella

Baada ya kuona Hali ya familia hiyo Hawa Kada makamu mweyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete amesema wao kama madiwani wataenda kuhakikisha mtoto huyo anapata bima kubwa itakayo wezesha kupata matibabu kila yanapohitajika ili kuwapunguzia gharama za matibabu wazazi.

The post UWT wamshika mkono kijana mwenye ulemavu wilayani Makete first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/f079OUI
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: UWT wamshika mkono kijana mwenye ulemavu wilayani Makete
UWT wamshika mkono kijana mwenye ulemavu wilayani Makete
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/01/172f802e-f373-48fd-9d21-2bfd71e864f4-950x534.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/uwt-wamshika-mkono-kijana-mwenye.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/uwt-wamshika-mkono-kijana-mwenye.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy